Monday, April 11, 2011

MTI WA MLONGE WENYE MAAJABU NA FAIDA ZAKE ZAIDI YA KUMI

UJUE MTI WA MLONGE NA FAIDA ZAKE ZAIDI YA KUMI
Na Ismail Mang'ola
Eileen Kasubi ni mtanazania wa kwanza mwanamke ambaye ni mjasiriamali wa kazi za mikono aliyefanikiwa kufanya utafiti juu ya mti MLONGE ambao umekuwa na faida kubwa hapa nchini na kufanikiwa kuzitambua zaidi ya faida kumi za mti huo unaopatikana kwa uchache hapa Tanzania.

Mjasiriamali huyu anaweka wazi namna ya MLONGE ulivyokuwa na faida lukuki lakini kubwa kuliko yote ni kwamba watanzania wengi bado hawajazitambua faida za mti huu ambao ni adimu kwa kiasi fulani hapa Tanzania licha ya wajasiriamali hawa kuhamasisha.

Bi. Kasubi anasema MLONGE ni mti wenye maajabu hasa katika matumizi yake kuanzia majani yake, magome,mbegu ambazozimekuwa zikitoa tiba, kinga pamoja na lishe, haya ndiyo maajabu ya mtyi MLONGE.

KAMPUNI YA Makai Moringa Enterprises inayodiri na mkakati huu wa kutafiti kwa kina zaidi juu mti Mlonge, Bi. Kasubi ambaye ni mkurugenzi wa Makai Moringa, anasema kwa miaka mingi akishirikiana na wafiti wenzake ambao ni wajasiriamali kutoka nchini Malawi na Kenya, wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzitambua faida ya mti huo na hivi sasa wanachopigania ni mtaji mkubwa ambao utaweza kuwaendeleza wajasiriamali wanaotafiti baadhi ya matumizi ya miti hapa Tanzania.

Mkurugenzi Kasubi anasema mafanikio ambayo anajivunia kuyapata katika utafiti wake juu ya mti huo Mlonge ni pamoja na kufanikiwa kuutambua kuwa ni miongoni mwa miti ambayo inatibu baadhi ya maradhi sugu kama vile ugonjwa wa kisukari ambao umekuwa tatizo katika maisha ya jamii ya ya kitanzania.

Bi.Eileen Kasubi anazianisha bidhaa zake zitokanazo na mti huo wa MLONGE ambapo anasema mafanikio ya mti huo na faida zake ni kama ifuatavyo: Majani ya mti wa MLONGE yakisagwa unga wake hutumika kwa lishe ya mwanadamu.

Anaendelea kusema katika hayo majani pia bado yanaweza kutibu na kukinga maradhi zaidi ya magonjwa 300 kitu ambacho unaonyesha maajabu ya kutibu na kutumika kama lishe.

Si hivyo tu, unga huo wa mlonge bado unanafasi kubwa kulinda afya ya mwanadamu pamoja na kurutubisha mifumo mbalimbali ya mwili
hapo ndipo utagundua MLONGE ni mti wa maajabu.

FAIDA ZA MBEGU ZAKE

Mbegu za Mlonge hutibu maradhi kama Malaria, Saratani ya tumbo, hupunguza sonona stress, huleta hamu ya kunywa maji, huongeza kinga ya mwili CD4s,

Mbegu hizo za mti huo wa ajabu bado zinahamasisha jamii kuamka na kuutambua umuhimu wa mti MLONGE kwa mbegu hizo hutoa mafuta ya kupikia pamoja na mafuta ya kujipaka mewilini kwa nyakati tofauti.

Kwa upande wa mafuta ya kupikia chakula Bi. Kasubi anasema mafuta yake ya kupikia huua sumu kwenye chakula yaani Bacteria na huondoa cholesterol. Mafuta ya kupaka mwilini yaani (Moringa Skin Care Oil).

Mlonge unaendelea kutoa faida kemkem kwa mtanzania na jamii yote duniani kwani umeweza kuwapendelea na wanamichezo kwa kutoa mafuta ambayo yanachua pindi mchezaji anapokuwa ameshikwa na misuli wakati akiwa anacheza, Bi. Kasubi anaainisha kwamba katika utafiti wa kampuni yake amefanikiwa kutambua faida nyingine ya matumizi ya mti huo baada ya kufanikiwa kutengeneza mafuta ya kuchua na kuondoa maumivu yatokanayo na kukaza kwa misuli ya mwili yaani (MORINGA MASSEGE OIL)ambayo huondoa maumivu ya mgongo, kiuno, miguu, hutibu baridi, na hupasha misuli joto.

Bado mti huo unazidi kushika nafasi za juu kabisa hasa pale mtafiti huyu mwanamke ambaye amepigana kwa miaka minane sasa tangu aanze kufanya utafiti kabla ya kuungana na wajasiriamali wenzake, pia amefanikiwa kugundua kuwa MLONGE unao uwezo wa kutoa sabuni za aina mbalimbali zikiwemo (Toilet soap) na kutibu magonjwa mengine mbalimbali kama vile ugonjwa wa ngozi, fangazi, chunusi, mba na hulinda ngozi kwa ,muda mrefu.

Kama hiyo haitoshi, bado mti wa mlonge unaendelea kutetea miti mingine ambayo bado haijafanyiwa utafiti na kampuni hiyo, Bi. Kasubi anasema katika utafiti wake amegundua kuwa mti wa MLONGE umeweza kutoa mafuta ya kupaka kwenye nywele na huiimarisha nywele vilivyo na kuzifanya kuwa na rutuba tofauti na mafuta mengine yatumikayo hapa nchini, huu ni MTI WA MAAJABU MLONGE, amesema Eileen Kasubi Mkurugenzi wa Makai Moringa (Mlonge) anayepatikana katika jengo la Pamba House karibu na Imalaseko Posta mjini Dar es Salaam.
Kwa mawasiliano mpigie simu na;+255 2135531/ +255 713 607408 /+255787 607408. Dar es Salaam Tanzania.

7 comments: