Monday, May 21, 2012

Naibu Waziri wa Eilimu na Ufundi Mhe. Philiph Mulugo akisoma risala iliyoandaliwa na wahitimu wa chuo cha Kiislam cha Ununio wakati wa Mahafali ya kwanza chuoni hapo yaliyofanyika May 20 mwaka huu, chuo hicho kipo Boko nje kidogo ya jiji la Dar Es Salaam. Picha Na Ismail Mang'ola / FBM 

NAIBU WAZIRI WA ELIMU AHIMIZA NIDHAMU VYUONI

Na Ismail Mang'ola

 

Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhe. Philiph mulugo amehimiza nidhamu kuwepo vyuoni na kusema zaidi masomo ya maadili yawe nguzo ili kupunguza mmonyoko wa maadili ambao hivi sasa havishikiki.

Mhe. Mulugo amekipongeza chuo cha ualimu cha Ununio Teachers College kinachotoa mafunzo ya ualimu na kusema, wahitimu wa chuo hicho wananidhamu hajapata kuona.

Akitoa kauli hiyo kwenye Mahafali ya kwanza tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mwaka 2010, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Chuoni hapo, Mulugo alisema amefarijika kuona wahitimu wakiwa na nidhamu pamoja na maadili mema aliyoyaona kwa wahitimu hao tofauti na alivyozoea kwa wahitimu wa vyuo vingine kwa kile alichodai kuwa kutokuwepo kwa zomeazomea katika chuo hicho.

Naibu huyo alisema walimu wanapaswa kusimama kidete kuhakikisha wanafundisha somo hilo ili kuinusuru familia zijazo ambazo hivi sasa baadhi ya jamii yetu imekuwa ikipotoka kwenye maadili huku wengine wakivaa milegezo hali ambayo inadhihirisha kuwa mtu huyo hakulelewa katika misingi yenye maadili.

Sambamba na hilo, mhe. Naibu Waziri pia amekitaka chuo hicho kuendeleza malezi mema kwa wanachuo wake na yenye kuzingatia mila na tamaduni ya kweli na kusisitiza walimu wa chuo hicho wasikome kufundisha suala zima la nidhamu kama walivyoanza hapo awali.

Naibu huyo alisema kwamba, kitendo cha wahitimu hao kupokea salamu za Takbir kama dini yao inavyowataka hakika kimemkuna kiasi cha nini afanye ili aweze kuwalipa fadhila za kujijenga kinidhamu kwa wahitimu hao, alibainisha Mhe. mulugo.

Aidha mhe. Mulugo amewataka wahitimu hao kuridhika na mazingira yoyote watakapopelekwa kufanya kazi bila kuangalia kuwa ni vijijini ama la, alisema hivi sasa walimu wengi wamekuwa wakikwepa kwenda kufundisha mikoani kwa kile alichidai kuwa ni mbali na familia zao zilipo.

Alisema endapo wahitimu hao kama watafuata mkumbo wa walimu wengine ambao wametokea katika vyuo ambavyo havifundishi masuala ya dini, hapo watakuwa wamepotea na watakuwa hawajaitendea haki taaluma yao kwani taaluma hiyo haichagui mahali pa kufanyia kazi wala eneo.

kutoka na nidhamu hiyo kwa wahitimu hao, mhe. mulugo alimtaka mwalimu anayefundisha somo la nidhamu aliyetambulika kwa jina la Ustadhi Juma nchia ambaye pia ni Makamu wa chuo, alimpongeza kwa jitihada zake hizo na kumpatia kiasi cha 30, 000 huku akimuahidi kitita kingine cha 470,000 kama motisha ya kutoa somo la maadili mema.

Hata hivyo Mhe. Mulugo ametoa onyo kali kwa wamiliki wa vyuo vyote ambavyo havina usajili na kutofuata taratibu, alisema endapo siku atakapobaini baina ya vyo hivyo, atavifungia na kuwanyang'anya leseni hali ambayo itawalazimu kutopata tena leseni ya kuanzisha vyuo.

 

No comments:

Post a Comment