Thursday, April 14, 2011

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu akichangia mada moja ya semina za bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Ismail Mang'ola 
Add caption

HAKI YA MAMA! BABU HAROUN ANATISHA NTWARA WALAHI

Inspecotr Haroun a.k.a babu ameonyesha uwezo wake kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya katika mji wa mtwara wakati alipoenda kufanya shoo ya kufa mtu na kuwafanya mashabiki hao pamoja na wapenzi wa miondoko hiyo kumtaiti asiondeke kwa kutaka awapagawishe na kibao chake cha milima na mabonde. Picha na Ismail Mang'ola aliyekuwa Mtwara.
Mbunge wa Singida Mashariki 'kulia akimpa pole mwandishi Pascal Mayala baada ya kusumbuliwa na mkono alipata ajali mwaka jana. Picha na Ismail Mang'ola wa watzedblog. 

Monday, April 11, 2011



Mkurugenzi wa Kampuni ya Makai Moringa (MLONGE ) Bi. Eileen Kasubi aliyeweza kutafiti faida na matumizi ya mti Mlonge na kufanikiwa kuzijua faida zake. Picha na maktaba ya WATZEDBLOGSPOT.

MTI WA MLONGE WENYE MAAJABU NA FAIDA ZAKE ZAIDI YA KUMI

UJUE MTI WA MLONGE NA FAIDA ZAKE ZAIDI YA KUMI
Na Ismail Mang'ola
Eileen Kasubi ni mtanazania wa kwanza mwanamke ambaye ni mjasiriamali wa kazi za mikono aliyefanikiwa kufanya utafiti juu ya mti MLONGE ambao umekuwa na faida kubwa hapa nchini na kufanikiwa kuzitambua zaidi ya faida kumi za mti huo unaopatikana kwa uchache hapa Tanzania.

Mjasiriamali huyu anaweka wazi namna ya MLONGE ulivyokuwa na faida lukuki lakini kubwa kuliko yote ni kwamba watanzania wengi bado hawajazitambua faida za mti huu ambao ni adimu kwa kiasi fulani hapa Tanzania licha ya wajasiriamali hawa kuhamasisha.

Bi. Kasubi anasema MLONGE ni mti wenye maajabu hasa katika matumizi yake kuanzia majani yake, magome,mbegu ambazozimekuwa zikitoa tiba, kinga pamoja na lishe, haya ndiyo maajabu ya mtyi MLONGE.

KAMPUNI YA Makai Moringa Enterprises inayodiri na mkakati huu wa kutafiti kwa kina zaidi juu mti Mlonge, Bi. Kasubi ambaye ni mkurugenzi wa Makai Moringa, anasema kwa miaka mingi akishirikiana na wafiti wenzake ambao ni wajasiriamali kutoka nchini Malawi na Kenya, wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzitambua faida ya mti huo na hivi sasa wanachopigania ni mtaji mkubwa ambao utaweza kuwaendeleza wajasiriamali wanaotafiti baadhi ya matumizi ya miti hapa Tanzania.

Mkurugenzi Kasubi anasema mafanikio ambayo anajivunia kuyapata katika utafiti wake juu ya mti huo Mlonge ni pamoja na kufanikiwa kuutambua kuwa ni miongoni mwa miti ambayo inatibu baadhi ya maradhi sugu kama vile ugonjwa wa kisukari ambao umekuwa tatizo katika maisha ya jamii ya ya kitanzania.

Bi.Eileen Kasubi anazianisha bidhaa zake zitokanazo na mti huo wa MLONGE ambapo anasema mafanikio ya mti huo na faida zake ni kama ifuatavyo: Majani ya mti wa MLONGE yakisagwa unga wake hutumika kwa lishe ya mwanadamu.

Anaendelea kusema katika hayo majani pia bado yanaweza kutibu na kukinga maradhi zaidi ya magonjwa 300 kitu ambacho unaonyesha maajabu ya kutibu na kutumika kama lishe.

Si hivyo tu, unga huo wa mlonge bado unanafasi kubwa kulinda afya ya mwanadamu pamoja na kurutubisha mifumo mbalimbali ya mwili
hapo ndipo utagundua MLONGE ni mti wa maajabu.

FAIDA ZA MBEGU ZAKE

Mbegu za Mlonge hutibu maradhi kama Malaria, Saratani ya tumbo, hupunguza sonona stress, huleta hamu ya kunywa maji, huongeza kinga ya mwili CD4s,

Mbegu hizo za mti huo wa ajabu bado zinahamasisha jamii kuamka na kuutambua umuhimu wa mti MLONGE kwa mbegu hizo hutoa mafuta ya kupikia pamoja na mafuta ya kujipaka mewilini kwa nyakati tofauti.

Kwa upande wa mafuta ya kupikia chakula Bi. Kasubi anasema mafuta yake ya kupikia huua sumu kwenye chakula yaani Bacteria na huondoa cholesterol. Mafuta ya kupaka mwilini yaani (Moringa Skin Care Oil).

Mlonge unaendelea kutoa faida kemkem kwa mtanzania na jamii yote duniani kwani umeweza kuwapendelea na wanamichezo kwa kutoa mafuta ambayo yanachua pindi mchezaji anapokuwa ameshikwa na misuli wakati akiwa anacheza, Bi. Kasubi anaainisha kwamba katika utafiti wa kampuni yake amefanikiwa kutambua faida nyingine ya matumizi ya mti huo baada ya kufanikiwa kutengeneza mafuta ya kuchua na kuondoa maumivu yatokanayo na kukaza kwa misuli ya mwili yaani (MORINGA MASSEGE OIL)ambayo huondoa maumivu ya mgongo, kiuno, miguu, hutibu baridi, na hupasha misuli joto.

Bado mti huo unazidi kushika nafasi za juu kabisa hasa pale mtafiti huyu mwanamke ambaye amepigana kwa miaka minane sasa tangu aanze kufanya utafiti kabla ya kuungana na wajasiriamali wenzake, pia amefanikiwa kugundua kuwa MLONGE unao uwezo wa kutoa sabuni za aina mbalimbali zikiwemo (Toilet soap) na kutibu magonjwa mengine mbalimbali kama vile ugonjwa wa ngozi, fangazi, chunusi, mba na hulinda ngozi kwa ,muda mrefu.

Kama hiyo haitoshi, bado mti wa mlonge unaendelea kutetea miti mingine ambayo bado haijafanyiwa utafiti na kampuni hiyo, Bi. Kasubi anasema katika utafiti wake amegundua kuwa mti wa MLONGE umeweza kutoa mafuta ya kupaka kwenye nywele na huiimarisha nywele vilivyo na kuzifanya kuwa na rutuba tofauti na mafuta mengine yatumikayo hapa nchini, huu ni MTI WA MAAJABU MLONGE, amesema Eileen Kasubi Mkurugenzi wa Makai Moringa (Mlonge) anayepatikana katika jengo la Pamba House karibu na Imalaseko Posta mjini Dar es Salaam.
Kwa mawasiliano mpigie simu na;+255 2135531/ +255 713 607408 /+255787 607408. Dar es Salaam Tanzania.

Friday, April 8, 2011

DK. KIFIMBO NI ZAIDI YA MCHUNGAJI AMBIKILE MWAISAPILE!

Dk. Haruna Mageo Kifimbo akiongea na waandishi wa habari juu ya tiba za Asili zinazoweza kutibu maradhi sugu kama ilivyovumbuliwa na mchungaji mstaafu Mabikile Mwaisapile wa Loliondo mkoani Arusha a.k.a Babu.
Picha na Ismail Mang'ola wa Watezdblogspot. 

Wednesday, April 6, 2011

Kesho ndio kesho Kilimani Holl ndani ya mji wa Dom na JAHAZI Morden Taarab

Ikumbukwe ya kwamba wale wakali na nguli wa miondoko ya mipasho hapa Bongo Mzee Yusuf pamoja na kundi lake zima la JAHAZI MORDEN TAARAB wana wa kunakshinakshi, wanatarajiwa kuangusha bonge la shoo mbele ya wasomi wa bongo wanaoratibu program za sheria yaani wabunge, watakuwa pamoja na jahazi katika kuwakonga nyoyo mashabiki na wapenzi wa muziki katika mkoa huo wa Dom. Shoo hiyo itapigwa katika ukumbi wa KILIMANI Aprili 7mwaka huu, washikadau wote mnakaribishwa na kiingilio chako uwe nacho sio kikubwa saaana hakika utafurahia kiasi hicho ulichokitoa.  

Sunday, March 27, 2011

ZUNGU NDANI YA APRM

Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Hassan Zungu akifanunua namna wakuu wa nchi za umoja wa Afrika watakavyokutana na kujadili mkakati huo ambao tayari umeshakamilika na kazi hivi sasa imeshaanza .Picha na Ismail Mang'ola. /WMB.

MHE. SHIBUDA NAYE AUKUBALI MPANGO HUO WA APRM.

Mbunge wa Maswa Magharibi Shibuda John Paul Magalle akichangia hoja juu ya APRM. Picha na Ismail Mang'ola/WBM.

WABUNGE SASA WAIKUBALI APRM.

Mbunge wa jimbo la ukonga Mhe. Eugen Mwaiposa akichangia moja ya hoja katika mkakati wa APRM ambapo kwa ujumla Bunge la Jamuhuri ya Muungano ulikubaliana na mpango huo ambao utazishirikisha na kuwakutanisha viongozi wakuu wa nchi za Afrika. Picha na Ismail Mang'ola/ WBM.

HUU MKAKATI HUONDOA UMASIKINI JAMANIII!

Katibu mtendaji wa APRM Bi. Rehema A. Twalb akifafanua namna mpango huo wa APRM utakavyozinufaisha nchi zilizomasikini. Picha na Ismail Mang'ola/ WMB.

HUU MPANGO MWENZIO NDIO KWANZA NAANZA KUUELEWA, KUMBE UNAMANUFAAE!

Mhe. Elizabert Mbowe kushoto akiteta jambo na Mbunge wa Maswa Magharibi kupitia kiti cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wakati wa semina ya kuihamasisha umma pamoja na mashirika mengine kujiunga na mapango huo wa APRM unaolenga kuleta maendeleo. Picha na Ismail Mang'ola./WMB.

Mashirika, taasisi, Bunge waukubali mpango maridhawa wa APRM.

Mhe. Mbunge Anna Abdalah akichangia hoja juu ya mkakati wa kujipima kwa kutumia utawala bora uliobuniwa na viongozi wa nchi za umoja wa African Peer Review Machanism { APRM }. Picha na Ismail Mang'ola /WMB.

Thursday, March 17, 2011

UHAKIKA WA SIMBA KUNYAKUA UBINGWA HAUNA MAJADILIANO: RAGE

Mwenyekiti wa Club ya Simba Ismail Aden Rage, amesema timu yake ya wekundu wa msimbazi Simba Sport Club imejihakikishia kunyakua ubingwa wa mwaka huu na kusema suala la kuutwaa ubingwa huo kwa mara nyingine hauna kipingamizi kwani hadi hivi sasa hakuna timu ambayo itawatambia wakali hao. Picha na Ismail Mang'ola. 
Kidoleni ana pete ya ndoa,Klabu yupo peke yake mbona mtihani kwa mama nanii.
Mazingira kama haya ni sehemu ya kupendezesha miji ama mji kwa wale ambao wamekuwa wakithamini mandhari kama hii iliyopo pembezoni mwa barabara ya Kawawa maeneo ya Morocco Hotel Magomeni jijini Dar es Salaam., maeneo mengi yamekuwa yakifyekwa na kuchomwa moto na wasiopenda mazingira mazuri na badala yake hujikuta mji kubaki wazi mithili ya jangwa kitu ambacho tunaweza kupigania halii isitokee, watanzania wanapaswa kuhakikisha hali inalindwa na kila anayejijua kuwa ni mtanzania. Picha na Ismail Mang'ola.

Wee Bi. Mkubwa! inamaana huna Hasband wako mahomu?.

Haya ni mambo ya wadau wa kumbi za burudani lakini mwenzangu na mie kama mambo haya huyahusudishi, hakiamungu huwezi kutoka hata kiduchu utaishia kuyasikia tu kwa wenzako lakini usipime.
Aunt Ezekiel akiwa katika moja ya pozi.
Msanii ghali wa muvi hapa tz Aunt Ezekiel akinena jambo na msanii mwenzake mishale ya saa tisa usiku katika ukumbi wa Mango jijini pale Twanga walipokuwa wakitoa burudani. Picha na Ismail Mang'ola.
Mnenguaji wa Extra Bongo ambaye jina lake halikufahamika moja akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki katika moja ya onyesho la bendi hiyo hapa jijini.

Kumbe Spaider nawe kwenye misafara ya Kenge umoooo! haya huku wapi tena, afu mbali kinoma na unakokaa duh.

Msanii wa muziki wa mduara Rashid Mustafa Msabaha (Spaider) kulia akiwa chobingo na mdu wake katika pande za Chang'ombe Unubini Temeke.
Tuesday Kihangala akigombania ugali na Stella ambaye ni msanii wa muvi hapa bongo.
Mwanamuziki wa kundi la Extra Bongo wana wa mbongo Mzee Faggason akiyarudi na shabiki wake alipokuwa akijinafasi na kundi hilo katika kile alichoahidi kuhakikisha anashuhudia mwenyewe kuliko kusimiliwa. 
                                     Picha na Ismail Mang'ola.

.Banza na Choki kunani?

  
Mafahari wawili ndani ya zizi moja, kulia ni Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki na kushoto ni Banza Stone mwanamuziki ghali hapa bongo.
Picha na Ismail Mang'ola.

Super Nyamwela akifanya vitu vyake kwa kushirikiana na madansa wenzake katika onyesho kali lililofanywa na kundi la Extra Bongo katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam.
RATIBA ya kundi zima la Extra Bongo wazee wa Vizigo kama vipi waite mabon town au ukuwapendelea zaidi unaweza ukawaita MJINI MIPANGO wanakushushia ratiba yao ya wiki watakapokuwa wanaporomosha burudani za kutosha ambazo kwa uhakika wengi wameweza kuzishuhudia.

Extra Bongo wiki hii wanatarajiwa kuimaliza hasa kwa kutumia zaidi Saikolojia. Ijumaa ya wiki hii wakali hao watashusha TSUNAMI ya kumalizia wiki katika ukumbi unaondana na wakati na uliotulia MEEDA uliopo Sinza jijini Dar es Salaam sambamba na nyimbo zao kali mpya ukiwemo MTENDA MTENDEWA.

RATIBA hiyo bado inasonga mbele ambapo siku ya Juma mosi kundi hilo litawasha moto mwingine katika ukumbi wa EQUATOR GRILL Mtoni kwa Azizi Ally.

KAMA KAWA ile siku ya Juma pili Kundi la EXTRA BONGO watafanya masababisho mengine katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni ambapo pia nyimbo kali zingine zitasikika siku hiyo, wakali wanaosababisha kunoga kwa muziki huo ni pamoja na nguli mwenyewe Ally Choki a.k.a Mzee wa Farasi ama Mzee Kijiko (GRADER), ama Mzee wa vibweka, usikubali kusimuliwa fika pale utakapowasikia wanatoa burudani.

Monday, March 14, 2011

HUWEZI AMINI!, HIVI ALIVYO ANATEGEMEWA NA MAMA YAKE MZAZI.

Mlemavu Balton Kiwelu ameelezea mstakabali wake juu ya hali aliyonayo na kusema licha ya ulemavu aliokuwa nao bado mama yake mzazi anamtegemea. Kiwelu amesema mama yake pia ni mlemavu ambaye alikatwa mguu wake mika mingi iliyopita na kumsababishia hali hiyo ya kutojishughulisha na badala yake akalitupia jicho lake kwa Balton. Watanzania, kutoa ni moyo, mwenye nacho asisite kumtafuta kwani anapatikana Liwiti / Msimbazi au barabara ya Bibi Titi Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na Ismail Mang'ola.

SEMINA YA WABUNGE WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UMEFUNGULIWA RASMI LEO.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa kampuni tata ya kufua umeme DOWANS katika ukumbi wa Blue Peal Hotel ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo. Picha na Ismail Mang'ola.

Sunday, March 13, 2011

MTU MZIMA KAZINI

Huyu ni askari wa kikozi cha Zima moto.
1.Nyumba moja ya Bw. Abdulkarim Sheru mkazi wa Mwananyamala Komakoma Kinondoni jijini Dar es Slaam, imenusurika kwa kuteketea na moto baada ya kutokea kwa kile kinachoaminika kuwa ni shoti ya umeme na kuteketeza vyumba vinne vya kulala na sebule mbili ambapo tathimini ya vitu vilivyoteketea bado haijafahamika.
Picha na Ismail Mang'ola. 

KILA KUKICHA MOTO MOTO

Gari lenye namba za usajili STK 2691 likiwa katika eneo la tukio mara baada ya kumaliza kuuzima moto huo.
Baadhi ya wapangaji wakiwaomba maafisa wa jeshi la polisi hawapo pichani kuingi ndani kuangalia kama kuna baadhi ya vitu vyao vilivyosalimika.



Abdkarim wa pili kutoka kushoto ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Bakharesa akihojiwa na maafisa wa jeshi la polisi, Tanesco na wengine kutoka kikosi cha Zima moto.  Picha na Ismail Mang'ola