Monday, June 4, 2012

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM

Amir wa Shura ya Maimamu Sheikh Mussa Kundecha akizungumzia juu ya Katiba mpya katika mkutano wa kuzindua waraka wa maoni ya Katiba hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond jubelee jijini Dar es Salaam. Picha na Ismail Mang'ola wa
www.fullutamu.blogspot.com/ FBM


JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM YATAKA MABOSI BARAZA LA
MITIHANI

Na Ismail Mang'ola/ FBM
 Jumuiya na Taasisi  za Kiislam Tanzania BARAZA KUU imemtaka Katibu wa Baraza la mitihani Taifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako na watendaji wake kuachia ngazi kwa kile kilichoelezwa kuwa wanahujumu matokeo ya mitihani ya wanafunzi wa kiislam.
Kauli hiyo ilitolewa jana kwenye mkutano wa kuzindua waraka wa maoni ya Katiba mpya na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya hiyo Sheikh Ramadhan Sanza.
Akizungumza katika mkutano huo Sheikh sanza alisema kwamba, kila mwaka wanafunzi wa kiislam wamekuwa na matokeo mabaya hali ambayo inatia shaka kutokana na uongozi wa baraza hilo ambao ni wa madhebu ya dini nyingine.
Sheikh Sanza alitaja mtiririko wa uongozi tangu kuanzishwa kwa baraza hilo kuanzia mwaka 1973 – 1977, alisema kuanzia mwaka huo hadi leo hii hakuna kiongozi ambaye ameshika nyadhifa za juu Katibu na Mwenyekiti akiwa muislam.
Aidha alisema sio nafasi hizo tu hata pia nafasi zinazofuata pia hakuna muislam ambaye alishawahi kushika ama kwa muda lakini wote wanaopangwa kuongoza kitengo hicho ni wa madhehebu mengine, alisema Sanza.
Alisema hali hiyo inaweza ikaleta mvurugano hasa endapo kama wataendelea kuona vijana wao wakiendelea kufanya vibaya wakati wakijua uwezo wao hali ambayo iliwapelekea wazazi wa wanafunzi hao pamoja na walimu wa masomo hayo kuamua kukata rufaa kwa kutokubaliana na matokeo hayo.
Alisema Baraza la Wakuu wa shule zaKiislam lilimwandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kumuomba aunde tume huru ya kuchunguza matokeo ya somo husika.
Sheikh Sanza alisema kwamba, kufuatia malalamiko hayo ya Wakuu wa shule za Kiislam, Barazala Mitihani liliyatizama matokeo hayo na kugundua kuwa walikosea, na hivyo Baraza hilo likaidhinisha kutolewa matokeo mapya ya somo hilo, ambapo mabadiliko hayo ya matokeo yalikuwa na athari kubwa kwa matokeo ya wanafunzi na shule zao, alisema Sanza.
Hata hivyo viongozi hao walilizungumzia sakata la Zanzibar na kusema kuwa, matukio yaliyotokea visiwani humo havihusiani na waislam ispokuwa ni kupakaziana ili muislam na mkristo watofautiane.
Sheikh Mapeo alibainisha baada ya manung’uniko yaliyopo hivi sasa midomoni mwa watu kudai kwamba, machafuko hayo yamefanywa na watu waonaomanika kuwa ni wa Jumuiya ya Kiislam (JUMIKa) kitu ambacho si kweli.
Alisema kwamba, ukweli utabainika endapo kama Serikali itaunda tume huru ya kuchunguza vurugu hizo zilianzia wapi na nani aliyeanzisha lakini hata hivyo akasema kuwa, makanisa yaliyochomwa moto yamechomwa na vijana wanaojiita polisi jamii.
Alisema vijana hao ndio wanaohusika moja kwa moja kuyachoma makanisa hayo moto na badala yake ikaonekana kuwa wanaUamsho ndio waliohusika kitu ambacho alisema hakina ukweli ndani yake zaidi ya kutaka kusababisha machafuko dhidi ya ndugu zao wakristo.
Sheikh Mapeo alihoji kwamba, ni matukio mangapi ambayo yamekuwa yakitokea visiwani Zanzibar na hakuna kanisa hata moja liliowahi kuchomwa moto, iweje leo waislam wafanye upuuzi huo wakati wakijua Qur’uan tukufu inawakataza kufanya hivyo?, alihoji Sheikh Mapeo.



No comments:

Post a Comment