WAISLAMU WALINDWA KAMA WAFALME
Polisi waongozwa kila walipohitaji kwenda Na Ismail Mang'ola
Licha ya Jeshi la Polisi nchini kuzuia maandamano ya watukufu Waislamu wakidai kupanguliwa kwa uongozi mzima wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kupigwa na marufuku na jeshi hilo, ajabu ya mussa ilionekana baada ya Waislamu hao kupingana na maamuzi yaliyotolewa na jeshi hilo na hatima yake maandamano yakawepo kama kawaida na cha kufurahisha zaidi, jeshi hilo lilitoa ulinzi wa kutosha kuwaongoza na kuwasikiliza watukufu hao nini hasa walichokuwa wakihitaji. Malengo na Madhumuni ya maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika katika kiwanja cha Kidongo Chekundu huku yakianzia katika Msikiti wa Kichangani Magomeni na kupiga kambi kwa muda mchache Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kisha kumalizikia katika kiwanja cha Kidongo Chekundu Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jeshi la polisi limeonyesha maajabu yake. Waislamu hao walijikuta wakipata ulinzi tofauti na matarajio yao ya awali baada ya kusikia kuwa maandamano hayo yamepigwa marufuku na kutolewa onyo kali la OLE WAO, onyo ambalo liliwanyong'onyesha wengi na kubaki majumbani wakijua hakutakuwa na maandamano tena, lakini baadaye wakashangaa kuona wenzao wakilindwa kama Wafalme kuanzia safari ilipoanzia Msikiti wa Kichangani hadi Kidongo Chekundu. Waislamu hao waliendelea kulindwa mithili ya Wafalme hao hasa pale baada ya kufika Kidongo Chekundu, Amiri wa Shura ya Maimamu Tanzania Sheikh Issa Ponda Issa, alipanda juu ya gari na kuanza kuwaelezea waumini wa Kiislamu waliofika katika kiwanja hicho nini hasa kilichowapelekea kufika na kukutana kiwanjani hapo. Wakati akianza kuelezea madhumini ya waislamu kuandamana na kuelezea kikwazo cha vijana wa Kiislamu kushindwa kuendelea na masomo ya juu na kuonekana suluhisho litakuwa wizara ya Elimu, Polisi waliwachukua baadhi ya viongozi wa jumuiya na Taasisi za Kiislamu akiwemo Sheikh Kondo kwenda Wizara ya Eilimu kupeleka madai yao. Kote huko Waislamu hao walikuwa wakilindwa, katika kiwanja cha Kidongo Chekundu halkadhalika polisi walikuwa wamekaa vizuri kiasi cha kumfanya kila aliyefika pale kujiona kuwa naye yupo katika hali salama, kuwepo kwa ulinzi wa kutosha.
|
No comments:
Post a Comment