Wednesday, October 28, 2015

UCHAGUZI MKUU MOTO. WAWILI WACHUANA VIKALI, NI EDWARD LOWASSA NA POMBE MAGUFULI

Wednesday, October 28, 2015

True value Media

 
 

Tume yatoa Ufafanuzi kuhusu ucheleweshwaji wa matokeo ya Urais

index 
………………………………………..
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji mstaafu Damian Lubuva ametoa ufafanuzi juu ya ucheleweshaji wa matokeo ya  awali ya ngazi Rais kutoka majimbo mbalimbali nchini.
Akitangaza matokeo hayo katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Oktoba 27, 2015  jijini Dar es salaam Jaji Lubuva amesema kuwa Tume inasubiri matokeo hayo kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kutoka katika majimbo yote nchini.
“waandishi wa habari mnatakiwa kuwa wavumilivu na kutangaza kile ambacho mnakisikia  na si kupotosha umma kwani Tume inatoa matokeo bila kupendelea chama chochote” aliongeza Jaji Lubuva.
Mbali na hayo jumla ya majimbo 87 yameshaleta majibu ya awali ya matokeo ya urais yakiwemo Mkoa wa Kusini Pemba Jimbo la Nchonga ambapo jumla ya wananchi 8,018 walijiandikisha, 5949 walipiga kura na kura halali zilikuwa 5771 ambayo ni asilimia 97.01 na 178.29 zilikataliwa.
Vilevile katika Jimbo la Chunguni waliojiandikisha walikuwa 13,416 ambapo wananchi 10,108 sawa na asilimia 75.34 walipiga kura, kura halali zilikuwa 9,792 sawa na asilimia 96.92 pamoja na kura 311 zilikataliwa ambayo ni sawa na asilimia 3.08.
Halikadhalika katika   Mkoa wa Mbeya Jimbo la Ileje jumla ya wananchi 56,002 walijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambapo asilimia 78.56 sawa na 43,997 walipiga kura, kati ya idadi hiyo kura 43,098 zilikuwa halali na kura 896 sawa na asalimia 2.04 zilikataliwa.
Jaji Lubuva aliongeza kuwa katika Jimbo la Ileje mkoani Mbeya ACT ilipata kura 501, ADC kura 347, CCM kura 26,368, CHADEMA kura 15, 651, CHAUMA walipata kura 155, NRA kura 26,TLP kura 36, pamoja na kura 20 kutoka chama cha UPDP.
Mbali na hayo majimbo mengine yaliyowakilisha matokeo hayo ni pamoja an Jimbo la Mtama kutoka Mkoa wa Lindi, Jimbo la Tunguu Mkoa wa kusini Unguja, Jimbo la kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, Jimbo la Nachingwea, Jimbo la mtama kutoka  mkoani Lindi, Jimbo la Mafia mkoani Pwani pamoja  Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani.
Pia Mkoa wa Katavi Jimbo la Mpanda vijijini, Mkoa wa Magharibi Mjini Jimbo la Fuoni, Jimbo la Kikwajuni, Jimbo la Mwera, Jimbo la Amani na Jimbo la Magomeni Mkoa wa Unguja Jimbo la Nungwi, Kaskazini Unguja Jimbo la Bumbwini, mkoa wa Rukwa Jimbo la nkasi kusini, Mkoa wa Kagera Jimbo la Nkenge na  Jimbo la Byalamuro, kutoka Mkoani Arusha Jimbo la Arusha Mjini yaliwakilisha matokeo yao.
Kwa upande wake Msaidizi wa  Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema Bwa. Matson Chizi  amesema kuwa mchakato mzima wa Uchaguzi ni mzuri wa wapo tayari kupokea matokeo hayo kwa jinsi yatakavyokuwa.

MATUKIO KUTOKA KATIKA UKUMBI WA MWALIMU NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM

1
Makamu Mwenyekiti Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Bw.Hamid M. Hamid (wapili kushoto) akisoma matokeo ya wagombea nafasi ya Urais leo jijini Dar es Salaam katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu,anayemfuata kulia ni Mwenyekiti  wa Tume Jaji  Mstaafu Damian Lubuva.
2
Baadhi ya waandishi wa Habari wa Ndani na  Nje ya nchi wakifuatilia zoezi la kutangazwa kwa matokeo ya wagombea Urais  katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu  leo katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
3
Msaidizi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema Bw. Matson Chizi akihojiwa na mwandishi wa habari wa Idhaa ya Kiswahili, Sauti ya  Ujerumani (DW) Bi.Hawa Bihoga  kuhusu namna gani analiona zoezi la utangazaji wa matokeo linafanyika.
4
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi  Jaji Mstaafu Damian Lubuva  wanne kushoto kwa waliyokaa katika picha ya pamoja kwa baadhi na waangalizi wa uchaguzi kutoka nchi za  Jumuiya ya SADC walipotembea ukumbi unaotumika kutangazia matokeo ya wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu leo jijini Dar es Salaam.
5
Mwandishi wa habari kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.Edward Kondela akimhoji mmoja wa waangalizi wa uchaguzi ambaye ni  Mwenyekiti wa SADC  nchini Malawi Bw.Justice Mbendera  alipotembelea ukumbi wa kutangazia matokeo ya urais leo jijini Dar es Salaam.
 Picha na Ismail Mang'ola

WALIOSAMBAZA MATOKEO YA URAIS KINYUME CHA SHERIA WAPANDISHWA KIZIMBANI MAHAKAMA YA KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (katikati), akizungumza na mmoja kati ya vijana nane waliofikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam leo, kwa tuhuma za kusambaza matokeo ya kura za mgombea nafasi ya urais wa chama hicho katika mitandao ya kijamii kinyume na utaratibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Imedaiwa vijana zaidi ya 190 walikamatwa kwa kosa hilo.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam leo.
Askari wa FFU wakiimarisha ulinzi mahakamani hapo.
Wafuasi wa Chadema wakionesha alama ya vidole viwili wanayoitumia.
Viongozi wa Chadema wakitoka katika mahakama hiyo baada ya kusikiliza kesi hiyo. 
Vijana waliokamatwa wakiwa katika mahakama hiyo.
………………………………………………………………..
 
Na Ismail Mang'ola
 
WATU wanane akiwemo Raia mmoja wa Korea na raia mmoja wa Kenya wamepandishwa kizimbani kwa kusambaza taarifa za matokeo ya urais katika Mtandao wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi yakiwa na kichwa ‘M4C election result management system’ bila kuthibitishwa kwa lengo la kupotosha umma. 
Sanjari na hilo, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), amewasilisha mahakamani hati ya kuzuia dhamana ya washtakiwa kwa kile alichadai kuwa ni kwa sababu ya usalama na kwa maslahi ya Taifa.
Washtakiwa hao ni Mashinda Mtei (49) mkazi wa Tengeru Arusha, Julius Mwita (40) mwanasiasa na ni mkazi wa Magomeni, Frederick Fussi (25) IT, mkazi wa Mbezi, Julius Matei (45) raia wa Kenya, Meshack Mlawa (25) mchungaji na ni mkazi wa Keko, Anisa Rulanyan (41) Mhandisi, mkazi wa Kawe, Jose Nimi (51) mkazi wa Uingereza na Kim Hyunwook (42) raia wa Korea.
Wakili wa Serikali Mkuu Edwin Kakolaki alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Respicius Mwaijage wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuwa washtakiwa wanashtakiwa kwa mashtaka matatu.
Ilidaiwa kuwa katika shtaka la kwanza linawakabili washtakiwa wote, ambapo inadawa kati ya Oktoba 25 na 26 mwaka huu, wakiwa katika vituo tofauti tofauti ndani ya jiji la Dar es Salaam walitoa taarifa za uongo kwenye mitandao wakati wakijua hazijadhibitishwa.
Kakolaki alidai washtakiwa hao walisambaza taarifa hizo kwenye mtandao huo na katika mitandao mingine ya kijamii ambayo ni  Facebook na Twitter kutangaza matokeo ya urais ya mwaka huku kwa lengo la kuposha umma huku wakijua hayajadhibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Katika shtaka la pili linamkabili Matei, Nimi na Hyunwook, ambapo wanashtakiwa kuwa Oktoba 26 mwaka huu wakiwa katika hoteli ya King iliyopo Kinondoni , Dar es Salaam wakiwa na hati za kusafirilia zenye namba A1532119, 930879 na M 27687807 walijiingiza katika ajira ya kukusanya na kusambaza matokeo ya urais ya uchaguzi wa mwaka huu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema ) bila kibali.
Pia, alidai katika shtaka la tatu lina mkabili Matei peke yake ambaye akiwa raia wa Kenya mwenye hati ya kusafirilia namba A1532119 akiwa ndani ya jiji  la Dar es Salaam alijihusisha na biashara katika Saccos ya Wanama bila kibali.
Baada ya washtakiwa hao kusomewa mashtaka hayo, walikana kuhusika na tuhuma hizo, ambapo Kakolaki alidai upelelezi bado haujakamilika na pia alidai DPP amewasilisha hati ya kuzuia dhamana kwa sababu ya usalama na maslahi ya Serikali.
Wakili wa washtakiwa hao Peter Kibatala, alidai kuwa mashtaka yanayowakabili wateja wake yanadhaminika, kwa hiyo aliiomba mahakama iwapatie dhamana.
Pia, alidai hati hiyo ya DPP haiko mahakamani hapo kihali na kuiomba Mahakama itupilie mbali hati hiyo kwa sababu haina mashiko kisheria.
Kibatala alidai kuwa hati ya mashtaka iko tofauti na hati ya DPP kutokana na kifungu kilichokuwepo kuwa si sahihi, kwa hiyo kama ni hivyo hati hizo zote hazifai, kutokana na mapungufu hayo.
Baada ya Kibatala kudai hivyo, wakili Kakolaki alidai kuwa hati ya DPP ipo kihalali mahakamani na anayuetakiwa kuthibitisha hilo na mahakama kwa hiyo waiyachie mahakama.
Alidai kuhusu kifungu kilichotumika ni sahihi, akaiomba mahakama itupilie mbali hoja za Kibatala na washtakiwa wanyimwe dhamana kwa mujibu wa sheria, baada ya DPP kuwasilisha hati hiyo.
Hakimu Mwaijage alisema uamuzi wa hoja hizo atazitoa Oktoba 30 mwaka huu na washtakiwa aliamuru warudishwe rumande.
Nje ya mahakama
Washtakiwa hao waliondoka katika eneo hilo la mahakama wakiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi ambapo wakiwa ndani ya magari ya polisi walikuwa wakionesha alama za vidole viwili.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salim Mwalimu, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sauti, Profesa Mwasiga Baregu na viongozi wengine wa Chadema walijitokeza mahakamani hapo kufuatilia shauri hilo.

MATOKEO RASMI YA WAGOMBEA URAIS TANZANIA MAJIMBO 26 USIKU



TANGAZO LA MSIBA WA MAMA JUDITH TARIMO

Familia ya Marehemu Cyprian Tarimo ya Ukonga, Mombasa Dar es Salaam inasikitika kutangaza kifo cha mama yao mpendwa Mama Judith Tarimo kilichotokea Oktoba 25,2015 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu Ukonga-Mombasa na Rombo Mahida, Mkoani Kilimanjaro. 
Habari ziwafikie ndugu jamaa na marafiki wote wa ukoo wa Tarimo na Shayo, popote pale wa lipo. 
Mwili wa marehemu unataraji kuagwa Oktoba 28,2015 kabla ya kusafirishwa siku hiyohiyo kwenda Mahida Rombo kwa maziko Alhamisi Oktoba 29,2015.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA YESU LIHIMIDIWE AMEN. 

TULINDE AMANI TUNAPOENDELEA KUPOKEA MATOKEO

 
Ndugu watanzania wenzetu, tunapenda kuwapongeza
kwa kumaliza mchakato wa kampeni za vyama vya siasa na wagombea  kwa
amani na utulivu. Vile vile tunawapongeza kwa kupiga kura kwa kwa amani
na utulivu, kwani pamoja na kujitokeza kwa wingi tulipiga kura kwa
kufuata sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi ukiachilia mbali kasoro
ndogo ndogo zilizojitokeza katika zoezi hilo. 
Ndugu watanzania wenzetu,  tangu juzi jumapili 25 Oktoba tulianza kupokea matokeo. Hiyo ni hatua muhimu sana kwa taifa letu, demokrasia yetu na amani ya nchi yetu. Wote tutakubaliana kwamba nchi nyingi za kiafrika zimeingia katika machafuko ya kisiasa na kuvuruga amani ya nchi hizo katika kipindi cha kupokea matokeo. 
Nchi za Ivory Cost iliingia katika mgogoro wa kisiasa kwa wakati wa kupokea matokeo, ikaingia katika mapigano  ya wenyewe kwa wenyewe maelfu ya wananchi walipoteza maisha, wengine wakijeruhiwa vibaya na wengi wakiyakimbia makazi yao. 
Mwaka
2007, Nchi jirani ya kenya nayo ilingia katika mgogoro wa kupokea
matokeo na hivyo kusababisha machafuko, watu zaidi ya elfu moja walipoteza maisha, wengi wakiachwa walemavu na maelfu wakiyakimbia makazi yao. 
Sisi
Global Peace Foundation Tanzania, tunaona mwenendo wa kupokea matokeo
ukianza kuingia dosari, kwa baadhi ya wagombea na wafuasi wa wagombea
kujitangazia matokeo. Ambao kwa Mujibu ka sheria ya uchaguzi ni kinyume,
ni kuvunja kanuni kwani chombo chenye dhamana ya kutangaza matokeo ni
Tume ya Taifa ya uchaguzi pekee. 
Kwa
sababu hiyo, tumeona tuwakumbushe wanasiasa na viongozi wa vyama vya
siasa kuwa wakati huu wanapaswa kuwa watulivu na waangalifu pindi
wanapotoa matamko. Kwa kufanya hivyo watakuwa wamewasaidia wafuasi wao
kuwa watulivu na hatimaye kutuvusha katika hatua hii tukiwa na amani na
utulivu. 
Tunaisihi tume ya uchaguzi ya Taifa NEC, na ile ya Zanzibar ZEC, kuharakisha mchakato wa kutangaza matokeo pindi yanapopatikana na kujumlishwa
ili kuepusha minong’ono na hisia hasi zinazoweza kupandikizwa kwa
wapiga kura na wananchi na baadaye kusababisha machafuko. 
Tunakiri kuwa pamoja na kuwapo migogoro ya hapa na pale, kuwepo kwa viashiria vya uvunjifu wa amani katika baadhi ya maeneo kama huko Unguja Zanzibar, baadhi ya maeneo ya Mbeya, Dar es Salaam na Lindi. Bado jeshi la polisi limeendelea kufanya kazi zake kwa weledi. Hata hivyo tunakisii chombo hicho kuwa waangalifu zaidi katika kipindi hiki adhimu kwani matumizi ya nguvu zilizopitiliza yanaweza kuchochea uvunjifu wa amani. 
Tunawakumbusha watanzania wenzetu mashabiki wa vyama vya siasa , wapiga kura na vyama vya siasa wajiandae
kupokea matokeo ya aina yeyote. kwani misingi ya kidemokrasia inatutaka
kuchagua na yule aliyepata kura nyingi ndiyo anakuwa mshindi. 
Na mwisho ni
kwa wanahabari na vyombo vya habari nyie mnabeba dhamana kubwa kwa
taifa hili katika wakati huu muhimu kwa taifa letu. Namna mtakavyotoa
taarifa kwa watanzania ndiyo itakayo amua mustakabali wa amani na
utulivu wa taifa hili. Mnalo jukumu na wajibu mahususi katika
kuhakikisha kuwa nchi hii inabaki salama, inabaki na umoja na
mshikamano, inabaki na utulivu. Toeni habari kwa kulingana na matakwa ya
taaluma yenu muhimu. 
Waswahili husema, sindano ya daktari huponya na kuua na kalamu ya mwandishi hujenga ama kubomoa. Kama ilivyo daktari
mwema, mwenye maadili huchagua kuponya na mwandishi makini atachagua
kujenga jamii yenye amani, utulivu na mshikamano kwa kutambua kuwa bila
amani hakuna maendeleo. 
Tunasimamia msemo wa watanzania uliopata umaarufu katika wakati huu wa uchaguzi kuwa KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI . Asanteni, Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania
 
Tafadhali bonyeza hapa chini kusikiliza wimbo maalumu wa kuhamasisha Amani ulioimbwa na Barnaba Boy 


MKWASA AITA 28 STARS KUIVAA ALGERIA

 
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi cha wachezaji 28 watakoingia kambini Jumapili jioni kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria Novemba 14 jijini Dar es salaam, na marudiano kufanyika Novemba 17 nchini Algeria.
Akiongea na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam, Mkwasa amesema kikosi chake hicho kitaweka kambi nchini Omani kwa takribani siku 10 kujiandaa na mchezo kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka 2018 dhidi ya Algeria.
Katika kikosi hicho, Mkwasa amewaita wachezaji wapya sita wakiwemo Salim Mbonde, Jonas Mkude, Salum Abubakar, Elias Maguri, Ramadhani Kessy na Malimi Busungu na kufanya idadi ya wachezaji 28.
Wachezaji aliowaita ni Magolikipa ni Ally Mustafa (Yanga), Aishi Manula (Azam), Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi wa pembeni Kessy Ramadhani, Mohamed Hussein (Simba), Juma Abdul, Haji Mwinyi (Yanga) na Shomari Kapombe (Azam), Walinzi wa kati ni Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub (Yanga).
Viungo ni Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar, Himid Mao, Mudathir Yahya, Frank Domayo (Azam), Jonas Mkude na Said Ndemla (Simba), washambuliaji wa pembeni Farid Musa (Azam), Saimon Msuva (Yanga) na Mrisho Ngasa (Free State Stars – Afrika Kusini).
Washambuliaji wa kati ni John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – Congo DR).
 

MO DEWJI FOUNDATION YATANUA MBAWA, YASAIDIA UBORESHAJI WA KITUO CHA FURAHINI MKOANI K’NJARO

User commentsBaadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakifurahia masomo wanayopatiwa ya kujiandaa na elimu ya sekondari katika kituo hicho cha Furahini mkoani Kilimanjaro.
……………………………………………..
Na Ismail Mang'ola
TAASISI ya misaada ya Mo Dewji Foundation imekubali kufadhili mradi wa kituo cha mafunzo cha vijana cha Furahini (FYLC) wenye lengo la kuboresha upatikanaji wa elimu katika kijiji cha Kisangara mkoani Kilimanjaro.
Imeelezwa kuwa taasisi hiyo ya bilionea Mo Dewji imetoa shilingi milioni 7 kusaidia ujenzi wa miundombinu inayotakiwa na kituo hicho chenye lengo la kuboresha elimu kwa watoto wa kijiji hicho.
Baadhi ya watoto hao ni wawafanyakazi wa mashamba ya Mkonge ya MeTL yaliyopo jirani na kijiji hicho.
Ufadhili huo unaenda sambamba na sera za MeTL za urejeshaji wa faida yake kwa wananchi kama sehemu ya wajibu wake kwa jamii, wenye lengo la kuimarisha ustawi wa jamii inayochangia biashara za kampuni hiyo.
Taasisi ya Mo Dewji ambayo ndiyo inatekeleza wajibu wa kundi la makampuni ya MeTL la kurejesha faida kwa umma, kwa ufadhili huo kwa kikundi cha Furahini wametanua wigo kutoka katika shughuli mbalimbaliw alizokuwa wakufadhili mkoani Singida.
Lengo la ufadhili huo ni kuwezesha jamii yenye kipato cha chini kabisa kuweza kumudu mikiki ya elimu ili kukabili umaskini.
Toka mwaka 2000 kundi la makampuni ya MeTL imekuwa ikitanua mazingira ya urejeshaji wa faida kwa umma kutokana na shughuli zake mbalimbali. Katika kipindi cha miaka mitano taasisi ya Mo Dewji imetumia zaidi ya dola za Marekani milioni 3 kusaidia miradi mbalimbali ya jamii.
User commentsBaadhi ya vijana hao wakiwa darasani wakiendelea na masomo katika jengo la kituo hicho cha Furahini ambacho kinatarajiwa kukabaratiwa na kwa msaada wa Mo Dewji Foundation.
Tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo, shughuli mbalimbali zimedhaminiwa na kufadhiliwa. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule, uchimbaji wa visima, ugawaji wa vyandarua, usambazaji wa unga wa mahindi kwa wananchi waliokumbwa na baa la ukame kwa mwaka 2005-2006,ufadhili kwa wanafunzi wa sekondari,afya kw awale waliozidiwa kiafya, kujenga kitengo cha macho katika hospitali za mkoa,kuweka taa katika mitaa, msaada wa chakula kwa waliokumbwa na ugonjwa wa ukimwi, ununuzi wa vifaa vya michezo na vifaa vya wakulima.
Kwa mujibu wa mratibu wa kituo hicho cha Furahini (FYLC) Bw. Msuya Isiaka, wazo la kuanzishwa kwa kituo lilitokana na uzoefu wa muda mrefu wa ufundishaji katika eneo hilo la mahusiano ya jamii.
Alisema wazo la kuanzishwa kwa kituo limetokana hasa na matokeo mabaya ya mitihani kwa wanafunzi wanoasoma shule za umma katika kijiji hicho.
“Elimu imekuwa tatizo kubwa katika jamii yetu hasa katika shule za serikali ambazo mara nyingi zimejikuta hazina walimu, na kama wakiwa wamebahatika wanakuwa na mwalimu mmoja wa somo la hisabati kwa shule nzima, bila kutaja masomo mengine kama fizikia, kemia na bayolojia,” alisema Isiaka na kuongeza kwamba kuna shida kubwa ya uwajibikaji kwa wlaimu na hivyo kluleta athari mbaya kwa wanafunzi.
“Tunaamini kwamba silaha yetu kubwa ya kukabili umaskini unaozunguka katika vizazi vyetu hapa Kisangara ni kuwa na elimu bora” alisema.
User commentsKwa mujibu wa Isiaka kituo hicho kinatakiwa kuwa na maktaba kamili na chumba cha tehama.
“Kwa kuwa na miundombinu hiyo ya kujifunzia ya maktaba na tehama, wanafunzi wanakuwa katika nafasi ya kujifunza vyema na kuwa katika hali ya kukabili umaskini unaozunguka janmii yetu.” alisema.
Mratibu huyo alisema kwamba mafunzo katika kituo hicho katika masomo ya kemia,fizikia,bayolojia na hisabati yalianza Juni 2015.
Kituo cha Furahini ambacho kimejengwa katika ardhi yenye ukubwa wa nusu eka katika kijiji cha Kisangara kata ya Mtuva katika wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjarokipo umbali wa kilometa 2.5 kutoka kituo cha mabasi cha Kisangara.
Kijiji cha Kisangara ambacho kipo katika eneo kame wastani kina wakazi wa kutoka makabila mbalimbali ambayo yalifika hapo kufanyakazi katika mashamba ya mkonge.
Mkonge ndio zao kubwa la biashara ambalo linalimwa na kampuni ya MeTL ikiajiri idadi kubwa ya watu kutoka katika kijiji hicho.
1 (11)Eneo la jengo hilo la kituo linavyoonekana kwa nje.
Ukame uliitafuta Kisangara kwa muda mrefu umesababisha kasi kubwa ya umaskini. Kutokana na hali hiyo watoto wameathirika zaidi kutokana na familia zao kushindwa kuwapeleka shule binafsi na kuwaacha katika shule za umma ambazo hazina ubora.
Kutokana na hali hiyo FYLC inajipanga kuhakikisha kwamba inarejesha matumaini kwa kuwawezesha wanafunzi hao kupunguza tofauti kati ya wanafunziw aosoma shule binafsi na shule za umma katika masomo.
Kituo kikiwa na wanafunzi 86 wa umri kati ya miaka 13 hadi 14 wanafundishwa kujiandaa kuingia kidtao cha kwanza kwa kufunzwa Fizikia, kemia,bayolojia,jiografia na Kiingereza.
Lengo kuu la kituo ni kuhakikisha kwamba wanawawezesha wanafunzi wanaosoma shule za umma wanakuwa na uwezo mkubwa kwa kuwapa nafasi ya kutumia maktaba na chumba cha Tehama na kuwapelekea walimu waliobobea kuwanoa wanafunzi hao na kuleta mabadiliko.
Aidha kituo kitatoa elimu ya maarifa ya afya ya uzazi kwa vijana ili kuweza kubadili maisha yao na kuondokana na tabia mbaya.
User commentsUkarabati wa kituo hicho ukianza baada ya Mo Dewji Foundation kukipiga tafu.
20151023_122610Mratibu wa Furahini Youth Learning Centre, Isiaka Msuya katika zoezi la kupakia matofali kwa ajili ya ukarabati wa kituo hicho kwa msaada wa Mo Dewji Foundation.

NI CCM JIJINI MWANZA.

Stanslaus Mabula akiongea na wanahabari baada ya kutangazwa mshindi wa Ubunge Jimbo la Nyamagana (CCM).
 
2
Ezekiel Wenje akiongea na wanahabari muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa.
3
Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jijini Mwanza Titho Mahinya akitangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu Jijini Mwanza.
4 
Kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana akiwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtaturu (kulia) muda mfupi kabla ya matokeo kutangazwa.
5
…………………………………………
Na Ismail Mang'ola, aliyekuwa Mwanza.

Mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza ameibuka mshindi wa kiti cha Ubunge katika jimbo hilo kwa kupata kura 81,017 na hivyo kumbwaga aliekuwa mbunge wa jimbo hilo Ezekiel Wenje kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema aliepata kura 79,280.
Matokeo hayo yalitangazwa na Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Jimboni humo ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Tito Mahinya huku kukiwa na Ulinzi Mkali wa vyombo vya ulinzi na usalama katika viunga vya ofisi za Jiji hilo.
Akitakangaza matokeo hayo majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo, Mahinya alibainisha kuwa pia CCM imeibuka kidedea kwa upande wa Madiwani ambapo kati ya Kata 18, imeshinda Kata 14 na Chadema Kata Nne.
Kwa upande wa Wagombea wengine, Chacha Okong’o (ACT Wazalendo) alipata kura 161, Faida Potea (CUF) amepata kura 1,005, Ahmad Mkangwa (NRA) kura 104, Mohamed Msanya (Jahazi Asilia) kura 175 na Ramadhan Mtoro (UDP) amepata kura 68.
Hata hivyo kabla ya matokeo hayo kutangzwa, Mgombea kutoka Chadema Ezekiel Wenje alikataa kusaini karatasi ya wagombea na kubainisha kuwa demokrasia haikutumika katika zoezi zima la uhesabuji wa kura katika uchaguzi huo na kwamba atafuata hatua zaidi za kisheria katika kupinga matokeo hayo.
Kwa upande wake Mshindi wa Uchaguzi huo Stanslaus Mabula alisema kuwa tangu awali alitarajia ushindi huo na kwamba suala la demokrasia limezingatiwa.
Katika hatua nyingine Mabula alibainisha kuwa atahakikisha anatatua changamoto zinazolikabili Jiji la Mwanza ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha wakazi wa Jiji katika shughuli mbalimbali za uzalishaji ili waweze kujitegemea kiuchumi.

MATOKEO YA WAGOMGEA URAIS MAJIMBO 11

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI YATANGAZA MATOKEO TENA KURA ZA URAIS KATIKA MAJIMBO KUMI (10), MAGUFULI APETA

1Y 2Y 3Y 4Y 5Y 6Y 7Y 8Y 9Y 10Y

Rais Kikwete akabidhi vitabu Chuo Cha ulinzi cha Taifa (National Defence College)

X1
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange vitabu kwaajili ya Chuo Cha ulinzi cha Taifa National Defence College(NDC) katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam  Oktoba 26, 2015.Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho cha NDC Meja Jenerali Gaudence Milanzi.
X2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue,Mkuu wa Majeshi ya ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,Mkuu wa Chuo Cha NDC Meja Jenerali Gaudence Milanzi wakiangali baadhi ya vitabu ambavyo Rais ameviakbidhi kwaajili ya matumizi ya Chuo hicho.
X3
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue(watatu kushoto),Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange,(kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Ulinzi Cha Taifa(NDC) Meja Jenerali Gaudence Milanzi(kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania muda mfupi baada ya Rais Kikwete kukabidhi vitabu kwaajili ya National Defence College) katika hafla iliyofanyika ikulu jijijini Dar es Salaam Oktoba 26, 2015.
(Picha na Ismail Mang'ola)

Rais Kikwete awaapisha Manaibu Katibu Wakuu na Katibu Tawala wa Mkoa

2
Naibu Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Ndugu Emannuel Kalobelo akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Oktoba 26, 2015.
 
 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  amewaapisha manaibu katibu wawili wa wizara na Katibu Tawala wa mkoa katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam Oktoba 26, 2015.Manaibu katibu walioapishwa ni pamoja Ndugu Emmanuel Kalobelo anayekuwa Naibu Katibu mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia na ndugu Tixon Nzunda nayekuwa Naibu Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.Katika hafla hiyo Rais Kikwete amemwapisha Mhandisi Madeni kipande kuwa katibu Tawala wa mkoa wa Katavi .
 
4
Naibu Katibu Mkuu mpya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ndugu Tixon Nzunda akila kiapo mbele ya Rais Kikwete.
5
Katibu Tawala mpya wa mkoa wa Katavi Mhandisi Madeni Kipande akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es salaam leo na kukabidhiwa miongozo ya kazi.
1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(wapili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na waliapishwa keo.Kushoto ni Katbu Tawala Mkoa wa Katavi Ndugu Madeni kipande, wanne kushoto ni Naibu katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Ndugu Emmanuel Kalobelo na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Mpya Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ndugu Tixon Nzunda.
Picha na Ismail Mang'ola

TUME YA UCHAGUZI YATANGAZA MATOKEO YA AWALI MAJIMBO MATATU

????????????????????????????????????

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akitangaza matokeo ya awali ya majimbo matatu kwenye ukumbi wa mikutano wa DICC jijini Dar es salaam huku akiwa ameongozana na wakurugenzi wa vitengo na maofisa zwa tume hiyo.  Jaji Lubuva ametangaza majimbo ya Paje Mkoa wa Kusini Unguja, Makunduchi na Jimbo la Lulindi mkoani Mtwara ambapo.PICHA NA ISMAIL MANG'OLA - JNICC -TUME YA UCHAGUZI -DAR ES SALAAM
????????????????????????????????????

Jaji Lubuva akiendelea kutangaza matokeo hayo wa tatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Ramadhan Kailima  na wa kwanza  ni Jaji Mstaafu Hamid Mahmod.
1t 2t 3t

HAFLA YA UTOAJI TUZO ZA NANI KAMA MAMA NA BALOZI WA HESHIMA WA LUGHA YA KISWAHILI AFRIKA 2015.

 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI), Dkt Ernesta Mosha akizungumza wakati wa hafla ya utoaji Tuzo ya heshima ya Balozi wa kiswahili Afrika  jijini Dar es Salaam.

????????????????????????????????????

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko akizungumza wakati wa hafla ya heshima ya Balozi wa kiswahili Afrika  jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (kushoto) akineonesha Tuzo aliyokabidhiwa kwa niaba ya Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete. Tuzo hiyo
ya Balozi wa heshima wa lugha ya kiswahili Afrika 2015 ni kutambua mchango alioutoa Mama Salma Kikwete katika kuendeleza lugha
ya Kiswahili ndani na nje ya Afrika. 
 Wageni waalikwa .
Wageni waalikwa .

WANAFUNZI 65 KUONDOKA KWA MASOMO NCHINI CHINA

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza na wazazi na wanafunzi wanaotarajia kuondoka Oktoba 28, 2015 kwenda kusoma masomo ya elimu ya juu wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam. 
Wazazi wakimsikiliza Abdulmaalik Mollel wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wazazi na wanafunzi  wanaokwenda nchini China kwa masomo ya elimu ya juu wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL), Abdulmaalik Mollel (hayupo pichani) wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL), Abdulmaalik Mollel akitoa nyaraka za taarifa za wanafunzi wanaokwenda nchini China wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam.
 Wanafunzi wakiuliza swali kwa masomo wanayokwenda kusoma katika vyuo vya nje wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Global Link Education (GEL), Abdulmaalik Mollel akizungumza na mzazi wa mwanafunzi wa anyekwenda kusoma nchini China wakati wa semina elekezi ya kuwajengea uwezo iliyofanyika makao Makuu ya GEL jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii.
…………………………………………………………………
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

KAMPUNI ya Global Link Education imeendelea kupeleka wanafunzi kwenda kusoma vyuo vya nje vilivyo na uwezo kutoa elimu bora.

Hayo ameyasema Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Link Education (GEL), Abdumaalik Mollel wakati akitoa mafunzo kwa wanafunzi 65 wanaokwenda nchini China kwa masomo ya elimu ya juu.

Mollel amesema vyuo vya nje ambavyo vinashirikiana na GEL vina ubora wa elimu pamoja na kuwa na vitendea kazi vinavyoweza kufanya mwanafunzi afanye vizuri katika masomo yao.

Amesema wanafunzi 500, GEL imesha wadahili katika vyuo vya nje na wanafunzi hao wameona ubora wa vyuo hivyo na kuweza kuleta chachu ya maendeleo nchini kutokana na utaalam wataopata huko.

Mollel amesema kuwa nafasi bado zipo katika vyuo vya China hivyo wazazi wanaweza kuwasiliana na GEL kufanya usajili katika vyuo hivyo.

“Nia ya GEL ni kuona wanafunzi wanafanya vizuri katika matokea na tunafatilia tabia zao hatua kwa hatua tukiwa na lengo ya kupata wasomi wenye ujuzi kwa maendeleo ya taifa”amesema Mollel.

Aidha amesema kuwa wanafunzi wanaonyesha tabia mbaya wanawarudisha nchini katika kuweza kuokoa fedha za mzazi kuendelea kuhudumia mtoto ambaye mwishoni hatafanya vizuri.

Wakazi wa Dar Wasimamisha Shughuli Kupiga Kura, Wajitokeza kwa Wingi

Wananchi na wakazi wa maeneo ya Tabata Liwiti wakiwa katika foleni ya kupiga kura leo jijini Dar es Salaam.
Wananchi na wakazi wa maeneo ya Tabata Liwiti wakiwa katika foleni ya kupiga kura leo jijini Dar es Salaam.
Wananchi na wakazi wa Tabata Shule wakiangalia majina yao kabla ya kupiga kura yao.
Mkazi wa eneo la Matumbi akipiga kura yake leo.
Mkazi wa Kawe akipiga kura yake leo.
Na Ismail Mang'ola, Dar es Salaam
WAKAZI wa maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam leo wamesimamisha shughuli zao na kushiriki zoezi la upigaji kura kuchangua viongozi wanaoona wanafaa kwa ajili ya kuwaongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Viongozi waliokuwa wakipigiwa kura leo ni wa ngazi ya udiwani, wabunge na nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Zoezi katika maeneo mengi ambayo mtandao huu ulitembelea ya Tabata, Ubungo, Sinza, Magomeni, Kigogo, Buguruni, Matumbi, Mwananyamala, Kawe pamoja na Kijitonyama zoezi limeenda vizuri huku idadi kubwa ya wapiga kura wakijitokeza kutimiza haki yao ya msingi.
Maeneo mengi vijana wameonekana kujitokeza kwa kiasi kikubwa huku vituo vingi vikitawaliwa na amani na utulivu katika vituo hivyo. Licha ya changamoto ndogondogo ambazo zilikuwa zikijitokeza kama baadhi ya wakazi kukosa majina yao kwenye orodha waliweza kupewa mwongozo ya nini cha kufanya na wasimamizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi.
Ramadhan Mabula ni Msimamizi wa Kituo Kata ya Ubungo akizungumzia eneo hilo alisema zoezi kwa kiasi kikubwa linaendelea vizuri na zipo changamoto ndogondogo ya baadhi ya watu kutoona majina yao lakini utatuzi umetolewa na ofisi za juu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na wanaendelea na zoezi vizuri.
Kwa upande wake Msimamizi Msaidizi wa vituo vya Kata ya Kigogo, Daudi Chambo alisema vituo vyote 59 vilivyopo sehemu mbalimbali katika Kata hiyo zoezi linakwenda vizuri na hata wananchi waliokuwa wakijitokeza kulalamika kutoona majina yao walisaidiwa na baadaye kupiga kura.
“…Unajua wapo waliokuwa wakilalamika hawaoni majina yao lakini ukifuatilia kiundani unakuta alikuwa akitafuta jina sehemu ambayo sio na aliposaidiwa aliweza kupiga kura na kuondoka,” alisema Chambo.
Licha ya idadikubwa ya wananchi kufika vituoni mapema zaidi yaani saa kumi za asubuhi na saa kumi na mbili zoezi limeanza majira ya saa moja asubuhi na wapiga kura kuendelea na upigaji kura huku wakiongozwa na wasimamizi na makalani vituoni. Katika vituo ambavyo vimetembelewa hakuna vilivyokwama kutekeleza shughuli hiyo ya upigaji kura.
Baadhi ya waangalizi wa uchaguzi wa ndani ya nchi wakijadiliana jambo wakiwa kazini katika kituo cha Tabata Liwiti.
Maeneo mengine foleni zilitembea haraka kiasi cha kumalizika mapema…
Eneo la Ubungo ambalo muda wote huwa na idadi kubwa ya watu na mishemishe nyingi leo lilikuwa shwari…
Foleni za wapiga kura eneo la Ubungo…
Baadhi ya waangalizi wa kimataifa wakifuatilia zoezi la upigaji kura kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam..
Foleni ya wapigakura Kata ya Ubungo..
Maeneo mengi ya jiji hata yale ambayo huwa yamechangamka leo yalikuwa yamesimamisha shughuli zake na watu kuelekea kutimiza wajibu na haki yao ya msingi ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowapenda. Mwandishi wa habari hizi ametembelea maeneo ya Ubungo, Sinza, Msasani, Kawe, Magomeni, Kinondoni na mengineyo ambapo idadi kubwa ya maduka yalikuwa yamefungwa na hakuna mikusanyiko ya watu hali inayoonesha wamesimamisha shughuli kutekeleza zoezi la kupiga kura.
Tayari vituo vingi vimehitimisha zoezi la upigaji kura na kujipanga kuanza kujumlisha kura kabla ya kutoa matokeo kama taratibu zinavyoelekeza. Endelea kuwa nasi tutakuletea matokeo kituo baada ya kituo kadri tunavyo yapokea.
Maeneo mengine makarani na wasimamizi waliwasubiri wapiga kura…
Foleni ya wapiga kura Mwananyamala Jijini Dar es Salaam…
Maeneo ambayo muda wote huwa bize leo hali ilikuwa ni tofauti, yaani yalikuwa kimyaaa kupisha zoezi la upigaji kura…
Wapiga kura na wakazi wa Kawe wakiendelea na zoezi hilo bila tatizo lolote…
Wananchi Kata ya Magomeni wakitimiza wajibu wao wa kuchagua viongozi…
Zoezi likimalizika eneo la Kituo cha Kigogo jijini Dar es Salaam…

UCHAGUZI DAR SHWAAAAAAARI

 Hali imekuwa shwari katika Jiji la Dar es Salaam hasa wakati wa upigaji kura kuwachagua madiwani, wabunge na Rais wa Awamu ya Tano. Jiji hilo lenye pilikapilika nyingi za maisha mfukuto mkubwa wa kisiasa lakini hali haikuwa hivyo bali ilitawaliwa na amani kila mahala. Pichani ni baadhi ya barabara zikiwa hazina misururu ya magari na vyombo vingine vya moto kama ilivyozoeleka.

 

 Hali ilivyokuwamchana wa leo  katika barabara za Morocco na Morogoro eneo la Magomeni Dar es Salaam.

 Kwenda Kinondoni kutoka Magomeni Mataa

 Kwenda Ilala, eneo la Mataa Magomeni

 Eneo la Banana Jimbo la Ukonga Dar

Hata wafanyabiashara hawakuwepo Banana, Ukonga Dar

WANANCHI WALIVYOJITOKEZA UPIGIAJI KURA JIJINI MWANZA.

Ni katika Vituo mbalimbali Jijini Mwanza ambapo zoezi la Upigaji Kura limeenda vyema huku likitawaliwa na utulivu katika vituo mbalimbali vya kupigia kura.
Na:George GB Pazzo
Katika Mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza hakukuwa na foleni za Magari kama ilivyozoeleka na hata shughuli nyingi zilisimama ili kupisha zoezi hili na muda si mrefu mbivu na mbichi zitaanza kujulikana hivyo ni vyema pande zote zikawa tayari kuyapokea matokeo kwani kwenye uchaguzi kuna kushinda na kushinwa.
Zoezi la upigaji kura limetawaliwa na utulivu wa hali ya juu katika vituo mbalimbali huku hamu ya kila mmoja kushiriki zoezi hilo ikiwa ni kubwa pia
Wakazi wa Jiji la Mwanza wakiendelea na zoezi la kupiga kura
Kulia ni Makoye Magige ambae ni Msimamizi Mkuuu wa Kituo cha Kitangiri Kati, eneo la Wazi namba Moja akiw-ongea na Wanahabari juu ya zoezi la uchaguzi katika kituo hicho ambapo amesema kuwa mambo yameenda shwari na hakukuwa na mapungufu makubwa mbali na baadhi ya wananchi kutotambua mapema majina yao yalipo katika Kata hiyo, japo changamoto hiyo imeshughulikiwa mapema.
Mwenye kofia ni Aloyce Mtani ambae ni Msimamizi wa Kituo cha Uchaguzi cha Bismack Jijini Mwanza akizungumza na Wanahabari
Kushoto ni Goodluck Masatu ambae niMtendaji wa Kata ya Kitangiri na msimamizi mkuu wa Uchaguzi katika Kata hiyo akiongea na Wanahari
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
Piga Kura kwa Amani
Zoezi la Kupiga kira likiendelea mapema hii leo
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
Wenye mahitaji maalumu nao wamepata usaidizi kwa uzuri kabisa
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Mwanza nao wameelezea namna zoezi lilivyooenda na baada ya kupiga kura walikuwa wakirejea majumbani mwao
BINAGI MEDIA GROUP, KWA PAMOJA TUIJUZE JAMII.
Kumbuka Uchaguzi Usitutenganishe, Zingatia Amani ndiyo Watanzania wanahitaji.

Rais Kikwete apiga kura Kijijini Kwake Msoga

1
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika foleni akisuburi zamu yake ya kupiga kura  katika kituo cha hospitali ya kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo  Oktoba 25, 2015.
2
Ofisa katika kituo cha kupigia kura katika kituo cha hospitali ya kijiji cha Msoga akihakiki kadi ya kupiga kura ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
3 4
Ofisa katika kitu cha kupiga kura akimkabidhi Rais Kikwete karatasi za kupiga kura.
5
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiandika kura yake ya siri.
7 8
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipiga kura ya Rais Mbunge na Diwani katika kituo cha kupiga kura cha hospitali ya kijiji cha Msoga,Kata ya Msoga wilayani Bagamoyo Oktoba 25, 2015.
9
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwekwa wino na msimamizi wa kituo unaotambulisha kuwa amepiga kura.
(Picha na Freddy Maro)  

MKE WA RAIS MAMA SALMA APIGA KURA KATIKA KITUO CHA MTANDA HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI.

Mama Salma Kikwete akisubiri kadi inayokaguliwa na msimamizi wa Kituo alichojiandikisha na hatimaye kupiga kura  katika Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Mtanda Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mjini.
Mama Salma akisubiri moja ya fomu za kuchagua Rais,Wabunge na Madiwani
Msimamizi wa kituo akiangalia picha ya Mama Salma katika dafutari la wapigakura
Mama Salma akiweka tiki kumchagua kiongozi BORA.
Mama Salma akitumbukiza karatasi ya kura ya Diwani.
Mama Salma akitumbukiza karatasi ya kura ya Mbunge.
Mama Salma akitumbukiza karatasi ya kura ya Rais.
Mama Salma akiwekwa vino na msimamizi wa kituo unaotambulisha kuwa amepiga kura.
Mama Salma akiwatakia kila la heri wananchi wanaotarajia kupiga kura kituoni hapo
Wananchi wakiwa katika mstari tayari kuelekea kupiga kura.
Wananchi wakiwa katika mstari tayari kuelekea kupiga kura.
Mama Salma akiagana na baadhi ya wananchi Uwanja wa Ndege wa Kikwetu Lindi.
Mama Salma akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Jordan Rugimbana.
Mama Salma akipanda Ndege  na kuwapungia mkono Maofisa waliopo Uwanja wa Ndege Kikwetu Lindi  tayari kuelekea Dar es Salaam baada ya kupiga kura.

WENGI WAJITOKEZA KUPIGA KURA KWA AMANI NA UTULIVU VITUO VYA NZASA,KENTONI, USTAWI WA JAMII NA MPAKANI ‘A’ KIJITONYAMA JIJINI DAR ES SALAAM.

Mmoja wa wakazi wa Kijitonyama mpakani akipiga Kura yake
KITUO CHA KUPIGIA KURA NZASA
Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Nzasa wakiwa wanangoja kupiga Kura
Bado wakazi wa Nzasa wanangoja kupiga Kura
Baadhi ya wakazi wakihakiki majina yao ili kujua wanatakiwa wakae sehemu gani kabla ya kupiga kura
Ulinzi pia ukiwa umeimarishwa hali ni Shwari
Leo shughuli zimesimama kupisha uchaguzi mkuu
Continue reading →

Kituo cha Segerea Magereza hali ni shwari Wengi wajitokeza kupiga kura

 Wakazi wa Segerea wakiwa katika foleni kwaajili ya kuendelea na zoezi la kupiga kura katika kituo cha Magereza Segerea muda huu huku hali ya usalama ikiwa shwari kabisa
 Foleni ikiwa bado ndefu huku mwamko ukiwa mkubwa kwa rika zote kuanzia vijana na wakina mama na baba zoezi linaendelea vizuri mpaka sasa
 Blogger Josephat Lukaza akiwa katika  foleni ya kupiga kura katika kituo changu cha Magereza segerea kwaajili ya kupiga kura kumchagua kiongozi atakayenifaa
Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog
 Wakazi wa Segerea ambao wamejiandikisha katika kituo cha Segerea Magereza wakiwa wamejitokeza kwa wingi muda huu katika kituo hiko kwaajili ya kushiriki zoezi la kupiga kura kuwachagua viongozi mbalimbali kuanzia Rais, wabunge na Madiwani. Hali ni shwari hakuna vurugu wala viashiria vyovyote vile vya vurugu japokuwa kuna changamoto za hapa na pale ambapo mkazi mmoja ameambiwa na msimamizi wa uchaguzi kuwa hawezi kupiga kura kutokana na namba ya Kitambulisho chake cha kupigia Kura kutofautiana tarakimu moja tu na Namba ya kitambulisho iliyoandikwa katika karatasi la majina ya kuhakiki. Mkazi huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema kuwa anasubiri Mkuu wa kituo cha Uchaguzi Segerea Magereza kuweza kuongea nae na Kutatua swala hilo endapo ataruhusiwa basi atapiga kura na asiporuhusiwa basi hatopiga kura
Wakazi wa Segerea wakiwa kwenye foleni kusubiri kupiga kura
Baadhi ya wakazi wa segerea wakiwa katika foleni tayari kwa kupiga kura.
Picha Na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Endelea kuwa nasi hapa tutakuletea kila kinachojiri kwenye vituo vilivyo karibu yetu

Waziri Mkuu Mizengo Pinda APIGA KURA KIJIJINI KWAKE KIBAONI

 unnamedm unnamedn
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akipiga kura kumchagua Rais, Mbunge na Diwani katika kituo cha kupiga kura kilichopo kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kibaoni wilayani Mlele Oktoba 25, 2015.
unnamedk
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiwa amembeba mototo aliyezaliwa usiku wa kuamkia tarehe 25,-10-2015  na kupewa jina la Magufuli katika kituo cha Afya cha Kibaoni wilayani Mlele Oktoba 25, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Nakumatt opens new Store in Uganda

unnamed1New PictureNakumatt opens 9th branch in Uganda, to further boost the local formal retail trade sector
25/10…Regional retailer, Nakumatt Holdings, has today opened the doors to its 9th branch in Uganda.
The opening of the new US$ 1.2million Nakumatt Naalya, located at Metroplex Shopping Mall further edges up Nakumatt’s regional network to 55 branches in Uganda, Kenya, Tanzania and Rwanda.
Speaking at the opening of Nakumatt Naalya, Nakumatt Holdings, Managing Director, Mr. Atul Shah, reiterated the firm’s commitment to foster regional trade integration by stocking locally sourced and produced products.
Having commenced its Uganda operations in 2011, Shah disclosed that Nakumatt, has successfully managed to raise its complement of Uganda manufactured products. In Tanzania, Nakumatt Tanzania, has also significantly increased its complement of locally sourced and manufactured products as it strives to raise the regional retail bar.
“Over the years, we have worked hand in hand with local manufacturers to raise the standards of locally manufactured retail products which now comprise more than 40% of our overall stocks across the region,” Shah said. Locally processed and manufactured products stocked at Nakumatt include foodstuff, cooking oils, detergents, assortedbeverages, fruits and vegetables.
The opening of Nakumatt Naalya, Shah noted, now sets the pace for the retailer’s ambition to close the year, with a complement of 60 branches in Kenya, Uganda, Tanzania and Rwanda.
At an estimated formal retail penetration rate of less than 20%, the regional formal retail market, Shah noted, is still a fledgling economic sector that deserves further support from the respective regional governments, to accelerate its growth.
“At Nakumatt, we are actively committed to our corporate mission, which is geared at boosting formal retail penetration in East Africa,” Shah said, adding, “The opening of Nakumatt Naalya, confirms the steadily growing demand for world class retail stores in Uganda, among other parts of East Africa.”
Covering a 35,000 square feet shopping floor area, Nakumatt Naalya, has been suitably furnished and stocked with a wide variety of retail products. The store, also features a distinct retail layout and ambience developed to guarantee a pleasurable shopping experience.
Fundamentally aligned to the retailer’s corporate mission, Nakumatt, Shah reiterated, is taking its in store retail experience to a whole new level. “All this, as we seek to maintain a distinct shopping ambience with the widest variety all under one roof,” Shah explained. “Complementing the in store ambience, we have also installed a range of energy efficient appliances,” he added.
The opening of Nakumatt Naalya, comes hot on the heels of the recent reopening of Nakumatt Westgate which now features a departmental store concept. The new departmental stores at Nakumatt Westgate, include a taste fully appointed Nakumatt Select (private brand) home furnishings concept store and the new Kids&Co Flagship Toys store alongside the Clarks and Skechers Lifestyle footwear stores. At Westgate Mall, Nakumatt Holdings is also piloting a Home&Décor, Home and Appliances, Food & Essentials and Sleep Centre Departmental Stores showcasing a variety of retail products.
Across the region, Nakumatt has maintained a trailblazers pace in the promotion of regional retail trade and now operates 9 branches in Uganda, 4 in Tanzania and 2 in Rwanda alongside its 40 stores in Kenya.
Alongside the store openings, Nakumatt is also actively enhancing its private brands (Nakumatt Select and Nakumatt Blue Label) rollout across the region.

NAAMINI UCHAGUZI UTAKUWA WA AMANI-WAZIRI MKUU Mizengo Pinda

index*Apiga kura, ataka Watanzania waendelee kumuomba Mungu
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema anaamini kwamba uchaguzi wa Rais,
wabunge na madiwani unaoendelea nchini kote leo, utafanyika wa amani
na utulivu.
Akizungumza mara baada ya kupiga kura leo asubuhi (Jumapili, Oktoba
25, 2015) katika kijiji cha Kibaoni, wilaya ya Mlele, mkoa wa Katavi,
Waziri Mkuu Pinda amesema hali aliyoiona tangu asubuhi inatia
matumaini.
Waziri Mkuu ambaye alipiga kura leo saa 3:10 asubuhi, alisema: “Watu
wamejitokeza kwa wingi. Ninawasihi Watanzania waendelee kumuomba Mungu
ili uchaguzi umalizike kwa amani. Lakini zaidi tuendelee kumuomba
Mungu ili amani tuliyonayo iendelee kudumu,” alisema.
Akizungumzia hali aliyoikuta kwenye kituo chake cha kupigia kura,
Waziri Mkuu alisema amefurahi kuona utaratibu mzuri uliopangwa wa
kutenganisha wapigakura. “Nimekuta akinamama wana mistari yao,
akinababa wana mistari na hapa kituoni kuna sehemu nne za kupigia
kura,” alisema.
Alisema kwa wastani mtu mmoja anatumia dakika mbili tangu kuhakikiwa
hadi kupiga kura. “Hii ni dalili njema kuwa kuna utaratibu mzuri na
kwamba watu watamaliza mapema kupiga kura,” alisema.
Aliwataka wapigakura kote nchini wakimaliza kupiga kura waende
majumbani kwao ikiwa ni kuitikia maelekezo ya Tume ya Taifa ya
Uchaguzi yanayowataka wananchi wasifanye mikusanyiko mita 200 kutoka
kwenye kituo cha kupigia kura.
Naye msimamizi wa kituo hicho ambaye pia ni Mtendaji wa Kata ya
Kibaoni, Bw. Thomas Senga alisema watu wamejitokeza mapema tangu saa 1
asubuhi. Alipoulizwa endapo mtu aliyesahau shahada yake lakini jina
lake lipo kwenye orodha ya waliojiandikisha ataruhusiwa kupiga kura,
alijibu kwamba mtu wa aina hiyo hataruhusiwa kupiga kura.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, OKTOBA 25, 2015.

DK. MAGUFULI APIGA KURA JIMBONI KWAKE CHATO

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli akipiga kura yake jimboni kwake Chato mapema leo asubuhi Oktoba 25, 2015.
(picha na Ismail Mang'ola).

MTONI KIJICHI, MBAGALA WENGI WAJITOKEZA KUPIGA KURA KWA UTULIVU NA AMANI JIJINI DAR ES SALAAM

 Rukia Omari (kushoto), akimsaidia kupiga kura jamaa yake Mwanaharusi Mohamed ambaye ni mlemavu wa macho wakati wa kupiga kura katika kituo cha Mbagala Misheni Dar es Salaam leo asubuhi.
  Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura katika Kituo cha Mtoni Kijichi Stendi Dar es Salaam leo asubuhi.
 Wananchi wakisubiri kupiga kura katika kituo cha Shimbwe Mbagala Kuu.
 Hapa wakihakiki majina yao.
 Mkazi wa Njia ya Ng’ombe Mbagala Kuu, Sarah Simba akipiga kura katika kituo cha Shimbwe Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kuwachagua viongozi wake, Rais, Mbiunge na Diwani.
 Wananchi wakiwa katika foleni ya kwenda kupiga kura katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mbagala Kuu.
 Wananchi wakiwa katika foleni ya kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Bwawani Mtoni Kijichi leo asubuhi.
 Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupiga kura katika Kituo cha Mtoni Kijichi Stendi Dar es Salaam leo asubuhi.
 Wasimamizi wa uchaguzi katika kituo cha Mbagala Misheni wakiwa kazini.
Msimamizi wa uchaguzi Mkuu katika kituo cha Mbagala Misheni, Yona Komba (kulia), akimpaka winoMwanaharusi Mohamed ambaye ni mlemavu wa macho baada ya kumaliza kupiga kura katika kituo hicho Dar es Salaam  leo asubuhi. Kushoto ni binti aliyemuomba amsaidie kupiga kura  Rukia Said.
 

MAKAMU WA RAIS DKT. MOHAMMED GHARIB BILAL APIGA KURA

unnamedMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitimiza wajibu wake wa kupiga kura kwa ajili ya kuchagua Rais, Mbunge, Mwakilishi, na Diwani kwenye kituo cha kupigia kura namba 7 katika Shule ya Sekondari ya Kiembesamaki Zanzibar, kwenye Uchaguzi Mkuu wa Tanzania unaofanyika leo Octoba 25, 2015 Nchini kote.
  












No comments:

Post a Comment