Wednesday, June 27, 2012

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...


Askari polisi wa Kituo cha Chang'ombe wakishusha mwili wa mtu katika Hospitali ya Temeke aliyekutwa amejinyonga Chamazi Manispaa ya temeke jijini Dar es Salaam, mwili huo ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitalini hapo. 
Picha na Ismail Mang'ola/ www.fullutamu.blogspot.com 


Wednesday, June 13, 2012

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...

Wape hao, wamezoea kufelisha ndugu zetu, huenda hata mimi nilikuwa na alama nzuri, sasa sijui nami nilichakachuliwa?, jamani Necta nini mnafanya, hii nchi siyo ya kidini sasa mbona mnataka kuleta udini? shauri yenu, au hamwajui Waislamu eee nyie hayeni tu. http://www.fullutamu.blogspot.com/ FBM/ 

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...


Haina ya kuandika tena si mnaona wenyewe hayo maandishi, hakika naamini kama ni ujumbe kwa wahusika hakika utakuwa umeshafika. Kaaaama kawaida inaitwa FBM/ www.fullutamu.blogspot.com/
By Ismail mang'ola


MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM

akinamama wa Kiislamu wakiwa katika kiwanja cha kidongo chukundu jijini Dar es Salaam wakifuatilia hatima ya vijana wao ambao wamekuwa wakihujumiwa alama za mitihani yao dhidi ya Baraza la Mitihani la Taifa, hivyo kuutaka uongozi mzima wa Baraza hilo lijiuzulu kuanzia nafasi ya Mwenyekiti, Katibu Mkuu pamoja na watendaji wake.
Picha na Ismail mang'ola wa FBM/ www.fullutamu.blogspot.com/ 

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM

Watukufu Waislamu wakimsikiliza kwa makini Sheikh Mapeo wakati akielezea kuhusu hujuma dhidi ya Watendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa NECTA katika maandamano yaliyofanyika siku chache zilizopita jinsi lilivyofanya hujuma kwa wanafunzi wa Kiislamu kwa kuwafyeka alama zao za mitihani. Picha na Ismail Mang'ola wa FBM/ www.fullutamu.blogspot.com

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM

  

WAISLAMU WALINDWA KAMA WAFALME
Polisi waongozwa kila walipohitaji kwenda
Na Ismail Mang'ola

Licha ya Jeshi la Polisi nchini kuzuia maandamano ya watukufu Waislamu wakidai kupanguliwa kwa uongozi mzima wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kupigwa na marufuku na jeshi hilo, ajabu ya mussa ilionekana baada ya Waislamu hao kupingana na maamuzi yaliyotolewa na jeshi hilo na hatima yake maandamano yakawepo kama kawaida na cha kufurahisha zaidi, jeshi hilo lilitoa ulinzi wa kutosha kuwaongoza na kuwasikiliza watukufu hao nini hasa walichokuwa wakihitaji.
Malengo na Madhumuni ya maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika katika kiwanja cha Kidongo Chekundu huku yakianzia katika Msikiti wa Kichangani Magomeni na kupiga kambi kwa muda mchache Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kisha kumalizikia katika kiwanja cha Kidongo Chekundu Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, jeshi la polisi limeonyesha maajabu yake.
Waislamu hao walijikuta wakipata ulinzi tofauti na matarajio yao ya awali baada ya kusikia kuwa maandamano hayo yamepigwa marufuku na kutolewa onyo kali la OLE WAO, onyo ambalo liliwanyong'onyesha wengi na kubaki majumbani wakijua hakutakuwa na maandamano tena, lakini baadaye wakashangaa kuona wenzao wakilindwa kama Wafalme kuanzia safari ilipoanzia Msikiti wa Kichangani hadi Kidongo Chekundu.
Waislamu hao waliendelea kulindwa mithili ya Wafalme hao hasa pale baada ya kufika Kidongo Chekundu, Amiri wa Shura ya Maimamu Tanzania Sheikh Issa Ponda Issa, alipanda juu ya gari na kuanza kuwaelezea waumini wa Kiislamu waliofika katika kiwanja hicho nini hasa kilichowapelekea kufika na kukutana kiwanjani hapo.
Wakati akianza kuelezea madhumini ya waislamu kuandamana na kuelezea kikwazo cha vijana wa Kiislamu kushindwa kuendelea na masomo ya juu na kuonekana suluhisho litakuwa wizara ya Elimu, Polisi waliwachukua baadhi ya viongozi wa jumuiya na Taasisi za Kiislamu akiwemo Sheikh Kondo kwenda Wizara ya Eilimu kupeleka madai yao.
Kote huko Waislamu hao walikuwa wakilindwa, katika kiwanja cha Kidongo Chekundu halkadhalika polisi walikuwa wamekaa vizuri kiasi cha kumfanya kila aliyefika pale kujiona kuwa naye yupo katika hali salama, kuwepo kwa ulinzi wa kutosha.












MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM


Mhe. Naibu Katibu Mkuu wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Selestine Gesimba akisaini Risala ya malalamiko ya Waislamu yaliyowasilishwa wizarani hapo hivi karibuni. Picha Na Ismail Mang'ola wa FBM/ www.fullutamu.blogspot.com 


Monday, June 4, 2012

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM

Amir wa Shura ya Maimamu Sheikh Mussa Kundecha akizungumzia juu ya Katiba mpya katika mkutano wa kuzindua waraka wa maoni ya Katiba hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond jubelee jijini Dar es Salaam. Picha na Ismail Mang'ola wa
www.fullutamu.blogspot.com/ FBM


JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM YATAKA MABOSI BARAZA LA
MITIHANI

Na Ismail Mang'ola/ FBM
 Jumuiya na Taasisi  za Kiislam Tanzania BARAZA KUU imemtaka Katibu wa Baraza la mitihani Taifa (NECTA) Dk. Joyce Ndalichako na watendaji wake kuachia ngazi kwa kile kilichoelezwa kuwa wanahujumu matokeo ya mitihani ya wanafunzi wa kiislam.
Kauli hiyo ilitolewa jana kwenye mkutano wa kuzindua waraka wa maoni ya Katiba mpya na Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya hiyo Sheikh Ramadhan Sanza.
Akizungumza katika mkutano huo Sheikh sanza alisema kwamba, kila mwaka wanafunzi wa kiislam wamekuwa na matokeo mabaya hali ambayo inatia shaka kutokana na uongozi wa baraza hilo ambao ni wa madhebu ya dini nyingine.
Sheikh Sanza alitaja mtiririko wa uongozi tangu kuanzishwa kwa baraza hilo kuanzia mwaka 1973 – 1977, alisema kuanzia mwaka huo hadi leo hii hakuna kiongozi ambaye ameshika nyadhifa za juu Katibu na Mwenyekiti akiwa muislam.
Aidha alisema sio nafasi hizo tu hata pia nafasi zinazofuata pia hakuna muislam ambaye alishawahi kushika ama kwa muda lakini wote wanaopangwa kuongoza kitengo hicho ni wa madhehebu mengine, alisema Sanza.
Alisema hali hiyo inaweza ikaleta mvurugano hasa endapo kama wataendelea kuona vijana wao wakiendelea kufanya vibaya wakati wakijua uwezo wao hali ambayo iliwapelekea wazazi wa wanafunzi hao pamoja na walimu wa masomo hayo kuamua kukata rufaa kwa kutokubaliana na matokeo hayo.
Alisema Baraza la Wakuu wa shule zaKiislam lilimwandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kumuomba aunde tume huru ya kuchunguza matokeo ya somo husika.
Sheikh Sanza alisema kwamba, kufuatia malalamiko hayo ya Wakuu wa shule za Kiislam, Barazala Mitihani liliyatizama matokeo hayo na kugundua kuwa walikosea, na hivyo Baraza hilo likaidhinisha kutolewa matokeo mapya ya somo hilo, ambapo mabadiliko hayo ya matokeo yalikuwa na athari kubwa kwa matokeo ya wanafunzi na shule zao, alisema Sanza.
Hata hivyo viongozi hao walilizungumzia sakata la Zanzibar na kusema kuwa, matukio yaliyotokea visiwani humo havihusiani na waislam ispokuwa ni kupakaziana ili muislam na mkristo watofautiane.
Sheikh Mapeo alibainisha baada ya manung’uniko yaliyopo hivi sasa midomoni mwa watu kudai kwamba, machafuko hayo yamefanywa na watu waonaomanika kuwa ni wa Jumuiya ya Kiislam (JUMIKa) kitu ambacho si kweli.
Alisema kwamba, ukweli utabainika endapo kama Serikali itaunda tume huru ya kuchunguza vurugu hizo zilianzia wapi na nani aliyeanzisha lakini hata hivyo akasema kuwa, makanisa yaliyochomwa moto yamechomwa na vijana wanaojiita polisi jamii.
Alisema vijana hao ndio wanaohusika moja kwa moja kuyachoma makanisa hayo moto na badala yake ikaonekana kuwa wanaUamsho ndio waliohusika kitu ambacho alisema hakina ukweli ndani yake zaidi ya kutaka kusababisha machafuko dhidi ya ndugu zao wakristo.
Sheikh Mapeo alihoji kwamba, ni matukio mangapi ambayo yamekuwa yakitokea visiwani Zanzibar na hakuna kanisa hata moja liliowahi kuchomwa moto, iweje leo waislam wafanye upuuzi huo wakati wakijua Qur’uan tukufu inawakataza kufanya hivyo?, alihoji Sheikh Mapeo.



MANG'OLA MEDIA .COM


Waumini wa Kiislam wakiwa katika ukumbi wa Diamond Jubelee katika mkutano wa kuzindua waraka wa maoni ya Katiba mpya na kuwataka Viongozi wakuu wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kujiuzulu mara moja kwa kile walichodai kuwa wanahujumu
 matokeo ya wanafunzi wa Kiislam. Picha na Ismail Mang'ola / FBM













Saturday, June 2, 2012

JINA LA KUITWA USTADHI LAMKERA MAKAMBA

Na Ismail Mang'ola

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Luteni mstaafu Yusuf Rajabu Makamba, amesema imefikia wakati naye aitwe sheikh badala ya hivi sasa anavyoitwa Ustadhi kutokana na mambo mengi ambayo amekuwa akiyafanya hasa yale yanayowahusu Masheikh.

 Bw. Makamba ameyabainisha hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa Karimjee wakati wa uzinduzi wa vitabu vyake BINADAMU NA KAZI na kile kinachokwenda kwa jina la UKWELI KWA MUJIBU WA BIBILIA NA KURU'AN TUKUFU ambavyo vilizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ghalib Bilal huku viongozi wengine wakihudhuria.

Kiongozi huyo alisema kwamba, hivi sasa kuna ulazima wa kuitwa Sheikh na sio Ustadhi tena kwa kuwa tayari ameshafanya mambo ambayo yalipaswa kufanywa na masheikhn kwa kutunga vitabu ambavyo vinahusisha makatazo ya kupokea na kutoa rushwa.

Aliendelea kuueleza uma uliofurika ukumbini hapo na kusema kwamba, kutokana na kuona jamii inazidi kupotoka na mambo mbalimbali yasiyokuwa na mafundisho, hivyo alilazimika kuingilia kati kazi za masheikh hao pamoja na maaskofu kuandika vitabu hivyo ambavyo hivi sasa wizara ya Elimu na Ufundi imeridhia wanafunzi wa darasa la tano (V) na la saba (VII) kujifunza mambo kadha wa kadha kupitia vitabu hivyo hasa kile cha BINADAMU NA KAZI.

Makamba alisema, awali vitabu hivyo vilizinduliwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa tanzania Fredrick Sumaye, lakini tangu hapo vilikuwa bado havijaanza kutumika rasmi lakini siku za hivi karibuni alifanya kila liwezekanalo ili vitabu hivyo vianze kutumika hasa mashuleni kwa ajili ya kuwapatia vijana wetu wanafunzi upeo na ufahamu kaatika mambo mbalimbali yaliyomo ndani ya vitabu hivyo.

 Mhe. Makamba alisema hivi sasa mwanadamu anatakiwa kufanya kazi kwa bidii zote ili kuleta mabadiliko kuliko kukaa na kucheza michezo ambayo haina mantiki na wala haitaweza kuwaletea faida yeyote katika maisha ya sasa, alisema na ndio maana watu wanamuona kila wakati anakuwa mkali, ukali huo unatokana na kuona watu wengi huwa hawapendi kujishughulisha na ndio maana anafikia hatua ya kuwakemea hata kama hawafahamiani kwa ukaribu.

Alikumbushia hata kipindi alipokuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaama, alisema alishawahi kufunga baa zote hapa mjini zile ambazo zilikuwa zikifunguliwa kuanzia asubuhi hadi usiku, alisema watu wengi walikuwa hawaendi makazini na badala yake wanashinda baa kwa kunywa kitu ambacho alikielezea kuwa huo ni uzembe na uvivu, alisema Luteni mstaafu Makamba.

Makamba alisema hivi sasa pamoja na kustaafu, lakini bado anajishughulisha ambapo kazi yake kubwa ni mfugaji wa Ng'ombe pamoja na kilimo huku mkewe akijishughulisha na ufugaji wa kuku, alisema Katibu huyo mstaafu.