Sunday, March 27, 2011

ZUNGU NDANI YA APRM

Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Hassan Zungu akifanunua namna wakuu wa nchi za umoja wa Afrika watakavyokutana na kujadili mkakati huo ambao tayari umeshakamilika na kazi hivi sasa imeshaanza .Picha na Ismail Mang'ola. /WMB.

MHE. SHIBUDA NAYE AUKUBALI MPANGO HUO WA APRM.

Mbunge wa Maswa Magharibi Shibuda John Paul Magalle akichangia hoja juu ya APRM. Picha na Ismail Mang'ola/WBM.

WABUNGE SASA WAIKUBALI APRM.

Mbunge wa jimbo la ukonga Mhe. Eugen Mwaiposa akichangia moja ya hoja katika mkakati wa APRM ambapo kwa ujumla Bunge la Jamuhuri ya Muungano ulikubaliana na mpango huo ambao utazishirikisha na kuwakutanisha viongozi wakuu wa nchi za Afrika. Picha na Ismail Mang'ola/ WBM.

HUU MKAKATI HUONDOA UMASIKINI JAMANIII!

Katibu mtendaji wa APRM Bi. Rehema A. Twalb akifafanua namna mpango huo wa APRM utakavyozinufaisha nchi zilizomasikini. Picha na Ismail Mang'ola/ WMB.

HUU MPANGO MWENZIO NDIO KWANZA NAANZA KUUELEWA, KUMBE UNAMANUFAAE!

Mhe. Elizabert Mbowe kushoto akiteta jambo na Mbunge wa Maswa Magharibi kupitia kiti cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wakati wa semina ya kuihamasisha umma pamoja na mashirika mengine kujiunga na mapango huo wa APRM unaolenga kuleta maendeleo. Picha na Ismail Mang'ola./WMB.

Mashirika, taasisi, Bunge waukubali mpango maridhawa wa APRM.

Mhe. Mbunge Anna Abdalah akichangia hoja juu ya mkakati wa kujipima kwa kutumia utawala bora uliobuniwa na viongozi wa nchi za umoja wa African Peer Review Machanism { APRM }. Picha na Ismail Mang'ola /WMB.

Thursday, March 17, 2011

UHAKIKA WA SIMBA KUNYAKUA UBINGWA HAUNA MAJADILIANO: RAGE

Mwenyekiti wa Club ya Simba Ismail Aden Rage, amesema timu yake ya wekundu wa msimbazi Simba Sport Club imejihakikishia kunyakua ubingwa wa mwaka huu na kusema suala la kuutwaa ubingwa huo kwa mara nyingine hauna kipingamizi kwani hadi hivi sasa hakuna timu ambayo itawatambia wakali hao. Picha na Ismail Mang'ola. 
Kidoleni ana pete ya ndoa,Klabu yupo peke yake mbona mtihani kwa mama nanii.
Mazingira kama haya ni sehemu ya kupendezesha miji ama mji kwa wale ambao wamekuwa wakithamini mandhari kama hii iliyopo pembezoni mwa barabara ya Kawawa maeneo ya Morocco Hotel Magomeni jijini Dar es Salaam., maeneo mengi yamekuwa yakifyekwa na kuchomwa moto na wasiopenda mazingira mazuri na badala yake hujikuta mji kubaki wazi mithili ya jangwa kitu ambacho tunaweza kupigania halii isitokee, watanzania wanapaswa kuhakikisha hali inalindwa na kila anayejijua kuwa ni mtanzania. Picha na Ismail Mang'ola.

Wee Bi. Mkubwa! inamaana huna Hasband wako mahomu?.

Haya ni mambo ya wadau wa kumbi za burudani lakini mwenzangu na mie kama mambo haya huyahusudishi, hakiamungu huwezi kutoka hata kiduchu utaishia kuyasikia tu kwa wenzako lakini usipime.
Aunt Ezekiel akiwa katika moja ya pozi.
Msanii ghali wa muvi hapa tz Aunt Ezekiel akinena jambo na msanii mwenzake mishale ya saa tisa usiku katika ukumbi wa Mango jijini pale Twanga walipokuwa wakitoa burudani. Picha na Ismail Mang'ola.
Mnenguaji wa Extra Bongo ambaye jina lake halikufahamika moja akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki katika moja ya onyesho la bendi hiyo hapa jijini.

Kumbe Spaider nawe kwenye misafara ya Kenge umoooo! haya huku wapi tena, afu mbali kinoma na unakokaa duh.

Msanii wa muziki wa mduara Rashid Mustafa Msabaha (Spaider) kulia akiwa chobingo na mdu wake katika pande za Chang'ombe Unubini Temeke.
Tuesday Kihangala akigombania ugali na Stella ambaye ni msanii wa muvi hapa bongo.
Mwanamuziki wa kundi la Extra Bongo wana wa mbongo Mzee Faggason akiyarudi na shabiki wake alipokuwa akijinafasi na kundi hilo katika kile alichoahidi kuhakikisha anashuhudia mwenyewe kuliko kusimiliwa. 
                                     Picha na Ismail Mang'ola.

.Banza na Choki kunani?

  
Mafahari wawili ndani ya zizi moja, kulia ni Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki na kushoto ni Banza Stone mwanamuziki ghali hapa bongo.
Picha na Ismail Mang'ola.

Super Nyamwela akifanya vitu vyake kwa kushirikiana na madansa wenzake katika onyesho kali lililofanywa na kundi la Extra Bongo katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam.
RATIBA ya kundi zima la Extra Bongo wazee wa Vizigo kama vipi waite mabon town au ukuwapendelea zaidi unaweza ukawaita MJINI MIPANGO wanakushushia ratiba yao ya wiki watakapokuwa wanaporomosha burudani za kutosha ambazo kwa uhakika wengi wameweza kuzishuhudia.

Extra Bongo wiki hii wanatarajiwa kuimaliza hasa kwa kutumia zaidi Saikolojia. Ijumaa ya wiki hii wakali hao watashusha TSUNAMI ya kumalizia wiki katika ukumbi unaondana na wakati na uliotulia MEEDA uliopo Sinza jijini Dar es Salaam sambamba na nyimbo zao kali mpya ukiwemo MTENDA MTENDEWA.

RATIBA hiyo bado inasonga mbele ambapo siku ya Juma mosi kundi hilo litawasha moto mwingine katika ukumbi wa EQUATOR GRILL Mtoni kwa Azizi Ally.

KAMA KAWA ile siku ya Juma pili Kundi la EXTRA BONGO watafanya masababisho mengine katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni ambapo pia nyimbo kali zingine zitasikika siku hiyo, wakali wanaosababisha kunoga kwa muziki huo ni pamoja na nguli mwenyewe Ally Choki a.k.a Mzee wa Farasi ama Mzee Kijiko (GRADER), ama Mzee wa vibweka, usikubali kusimuliwa fika pale utakapowasikia wanatoa burudani.

Monday, March 14, 2011

HUWEZI AMINI!, HIVI ALIVYO ANATEGEMEWA NA MAMA YAKE MZAZI.

Mlemavu Balton Kiwelu ameelezea mstakabali wake juu ya hali aliyonayo na kusema licha ya ulemavu aliokuwa nao bado mama yake mzazi anamtegemea. Kiwelu amesema mama yake pia ni mlemavu ambaye alikatwa mguu wake mika mingi iliyopita na kumsababishia hali hiyo ya kutojishughulisha na badala yake akalitupia jicho lake kwa Balton. Watanzania, kutoa ni moyo, mwenye nacho asisite kumtafuta kwani anapatikana Liwiti / Msimbazi au barabara ya Bibi Titi Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na Ismail Mang'ola.

SEMINA YA WABUNGE WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UMEFUNGULIWA RASMI LEO.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa kampuni tata ya kufua umeme DOWANS katika ukumbi wa Blue Peal Hotel ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo. Picha na Ismail Mang'ola.

Sunday, March 13, 2011

MTU MZIMA KAZINI

Huyu ni askari wa kikozi cha Zima moto.
1.Nyumba moja ya Bw. Abdulkarim Sheru mkazi wa Mwananyamala Komakoma Kinondoni jijini Dar es Slaam, imenusurika kwa kuteketea na moto baada ya kutokea kwa kile kinachoaminika kuwa ni shoti ya umeme na kuteketeza vyumba vinne vya kulala na sebule mbili ambapo tathimini ya vitu vilivyoteketea bado haijafahamika.
Picha na Ismail Mang'ola. 

KILA KUKICHA MOTO MOTO

Gari lenye namba za usajili STK 2691 likiwa katika eneo la tukio mara baada ya kumaliza kuuzima moto huo.
Baadhi ya wapangaji wakiwaomba maafisa wa jeshi la polisi hawapo pichani kuingi ndani kuangalia kama kuna baadhi ya vitu vyao vilivyosalimika.



Abdkarim wa pili kutoka kushoto ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Bakharesa akihojiwa na maafisa wa jeshi la polisi, Tanesco na wengine kutoka kikosi cha Zima moto.  Picha na Ismail Mang'ola

Friday, March 11, 2011

Mashuhuda wa ajali hiyo wakijinafasi kitoweo cha bwerereeeeee! hakika ama kweli kufa kufaana.
Picha na Ismail Mang'ola.

EXTRA BONGO WAKALIA KITI CHA KIFALME

1.Kundi la muziki wa dansi hapa nchini Extra Bongo hivi sasa limekaa mahala pazuri baada ya kufanikiwa kukikalia kiti cha Kifalme kwa kuzikamata baadhi ya kanda zinazohusudu burudani hiyo hasa katika kanda za Tabata, Kawe na maeneo mengine.

2.Nguli wa miondoko ya dansi Ally Choki akiwaburudisha mashabiki wa muziki huo katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam. Picha na Ismail Mang'ola.