Thursday, March 17, 2011

UHAKIKA WA SIMBA KUNYAKUA UBINGWA HAUNA MAJADILIANO: RAGE

Mwenyekiti wa Club ya Simba Ismail Aden Rage, amesema timu yake ya wekundu wa msimbazi Simba Sport Club imejihakikishia kunyakua ubingwa wa mwaka huu na kusema suala la kuutwaa ubingwa huo kwa mara nyingine hauna kipingamizi kwani hadi hivi sasa hakuna timu ambayo itawatambia wakali hao. Picha na Ismail Mang'ola. 
Kidoleni ana pete ya ndoa,Klabu yupo peke yake mbona mtihani kwa mama nanii.
Mazingira kama haya ni sehemu ya kupendezesha miji ama mji kwa wale ambao wamekuwa wakithamini mandhari kama hii iliyopo pembezoni mwa barabara ya Kawawa maeneo ya Morocco Hotel Magomeni jijini Dar es Salaam., maeneo mengi yamekuwa yakifyekwa na kuchomwa moto na wasiopenda mazingira mazuri na badala yake hujikuta mji kubaki wazi mithili ya jangwa kitu ambacho tunaweza kupigania halii isitokee, watanzania wanapaswa kuhakikisha hali inalindwa na kila anayejijua kuwa ni mtanzania. Picha na Ismail Mang'ola.

No comments:

Post a Comment