Wednesday, May 23, 2012

MANG'OLA MEDIA.COM

Huu ni muonekano wa mlima Meru. Picha kwa hisani ya www.fullutamu.blogspot.com/ FBM

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...

Ni sehemu ya mji wa Arusha a.k.a Half London jiji la maraha, jiji lililotulia, maisha yake kama unyamwezini mitaa ya kwa Obama, ukicheki kwa mbaali unauona mlima Meru, karibuni sana A Town, ndio kwetu jamani. Picha kwa hisani ya www.fullutamu.blogspot.com/ FBM

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...

Kaka angalia mateke, anapiga mateke huyo! kama Brucelee, au jeti lee' hu haa' yung 'yauo ,agopa sana. picha kwa hisani ya www.fullutamu.blogspot.com/ FBM 

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...


Unaitwa mlima KHARAA
Picha na www.fullutamu.blogspot.com/ FBM inawakilisha. 


MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...


Mwaka huu kwakweli home mambo si mabaya sana, chakula kipo kiukweli, nasema hakuna matata, kula kunywa kama kawa, kama dawa ni Manyara huko mtu wangu/ www.fullutamu.blogspot.com inawakilisha FBM/  


MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...

Waooo Josee na Maryy wajukuu zangu hakika mmetulia, lakini meryy mkorofi weweee, sema nawatakia maisha mema na makuzi bora, hapa ni mwanzo tu wa maisha yenu kikubwa ni kuangalia namna mtakavyoweza kujilinda na maisha magumu ya baadaye wajukuu zangu, nawaambieni kitu kimoja, msije mkasahau elimu, hakuna kilicho kizuri hapa ulimwenguni kama elimu, mtakapokuwa na elimu hakika mtakuwa wafalme wa kila idara, Peace & Love www.fullutamu.blogspot.com/ FBM inawakilisha.

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...

d
Dogo uko juu sana, hilo ni moja ya pozi ambalo nilishawahi kumuona mtu mmoja nchini Canada wakati nilipokuwa nikitafuta maisha baada ya kuzamia meli moja ya wagiriki, hongera sana dogo J, komaa jembe maisha ndio haya, ukiyachezea utakuja jijutia, nakusihi zaidi fikiria elimu, elimu ndio ufumbuzi wa maisha yako mwanangu' nakuthamini Juma. www.fullutamu.blogspot.com/ FBM inawakilisha.


MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...


Siku moja bwana nilikuwa pande za Mkoa wa Tanga, wakati nikiwa katika mtaa mmoja barabara ya 17, nikawakuta akina mama wa kisambaa wakiwa wanauza ndizi mbivu, nikatoa noti ya shilingi mia tano na kumkabidhi mmoja wa wauza ndizi na kisha akanipatia ndizi tano, mara akaja mzungu, akamuuliza yule mama aliyeniuzia ndizi. How Murch bananas.
akiwa na maana ndizi shilingi ngapi, yule mama wa kisambaa akamjibu "Baba hazijabanana nimatonga mafungumafungu' yaani maana yake 'Ndizi hazija banana bali amepanga mafungu mafungu! wee acha nicheke, nilicheka nilicheka, mara yule mzungu naye akaanza kuniiga kucheka, basi tena. www.fullutamu.blogspot.com/ kama kawaida ya FBM    


MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...

Hivi nyie hamjui kama Sigara ina Nicotin, madhara yake weeee mwenzenu nimekaribia kuiacha! Kama kawaida www.fullutamu.blogspot.com inawakilisha kila kona FBM/ 

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...


Thubutuuuu! ulipatie wapi, ingekuwa kama SANLG kweli ningekupigia saluti, lakini chombo hiki! wala hata sihangaiki, mambo ya mkwanja ndugu!
Kama kawaida yangu www.fullutamu.blogspot.com FBM


MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...


Kaaaama kawaida ya blog hii, kuwa nalo bado sana, lakini sina muda mrefu kihivyo' mbona maduuu wataniko........ www.fullutamu.blogspot.com/ FBM/


MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...

Weweee! mambo iko huku bana, dah mimashine ya ukweli, masaa mawili tu nipo home A Town, bila hata ya kusimama njiani, moja ya pikipiki inayouzwa bei mbaya sana hapa bongo, lakini ukienda nchi kama vile unyamwezini, aaah bukubuku kama mia tano hivi unaigomboa. acha kabisa. http://www.fullutamu.blogspot.com/ inawakilisha. FBM/

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA...


Una hela wewe la kuligomboa hili, we komaa na mingarangara yako' mpango mzima huu hapa, osha macho sasa, lakini angalia usije ukaiba mihela ya mdingi afu ukakimbilia mamtoni kwenda kulisaka, ligari kama hili, usipime babake.
kama kawaida, www.fullutamu.blogspoti.com inawakilisha. FBM/


MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM


Si mchezo babake, cheki mashine hiyo, ni mtukutuku wa ukweuuuu, mdude kama huu wala hautakuwa na haja tena ya kununua gari, kwanza yenyewe gari, inasemekana bei yake unaweza ukanunua wilaya moja kati ya wilaya tatu zilizopo hapa Dar, baba ushirikiano mwema.
FBM Inawakilisha. 


MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: Naibu Wa...


Wanavyuo na wanafunzi wa ngazi zote wametakiwa kufanya chaguzi za viongozi wa wanafunzi vyuoni, mashuleni. Picha na www.fullutamu.blogspot.com


Tuesday, May 22, 2012

MANG'OLA MEDIA .COM

Akina mama wa Kiislam wakifuatilia jambo katika Mahafali ya wahitimu wa Ualimu katika Chuo cha Ununio yaliyofanyika mwishoni mwa wiki hii. Picha na FBM / 

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: Naibu Waziri wa Eilimu na Ufu...

Mhe. Punguza mawazo, mbona jukumu lenyewe la kuwatunukia wahitimu wako sio gumu sasa unawaza nini mkuu? ina maana huku ulikowahi kupita hawakuwa na nidhamu kama hawa?
By.  FBM / 

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: Naibu Waziri wa Eilimu na Ufu...

Amina pokea zawadi hiyo, hakika nafikiri ni yako, ndugu zako wamependa na kufurahi sana kwa kuhitimu kwako, nasema allah atakuongezea neema na utazidi kupata mengi na ya kheri. Picha na FBM/

MANG'OLA MEDIA .COM: Naibu Waziri wa Eilimu na Ufundi Mhe. Philiph Mulu...


Baadhi ya wanafunzi ambao bado wanaendelea kutafuta elimu wakiwashuhudia wenzano namna wanavyotunukiwa vyeti vyao katika Mahafali hayo.
Picha na ismail Mang'ola FBM/


MANG'OLA MEDIA .COM: Naibu Waziri wa Eilimu na Ufundi Mhe. Philiph Mulu...

Amina hongera kwa juhudi nzuri ulizozifanya, dada elimu ni muhimu kuliko unavyofikiria, kaza buti nafasi bado ni yako, lakini nakushauri angalia usije ukabweteka na hicho cheti, mambo yote Digreee dada huko ndiko kwenye mpango mzima wa maisha, Asalam alayqum.
Picha na FBM/

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: Naibu Waziri wa Eilimu na Ufu...


Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Philiph Mulugo akitoa fedha Tsh: 30,000 kwa ajili ya kumpa zawadi mwalimu wa somo la Nidhamu na maadili mema Makamu wa chuo hicho Ustadh Juma nchia baada ya kufarahi kutokana na nidhamu na maadili mema waliyokuwa nayo wahitimu wa chuo hicho ambapo Mhe. alimuahidi makamu huyo kuwa mwishoni mwa mwezi huu atampa tsh:470,000 ambazo jumla ni 500,000.
Picha na FBM/


MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: Naibu Waziri wa Eilimu na Ufu...

Mkuu wa Chuo cha Ualimu Cha (Ununio Teachers College) akisoma risala katika Mahafali ya Chuo hicho yaliyofanyika May 20 / 2012 , Mhe. Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi aliwatunukia wahitimu Vyeti ngazi ya Cheti na Diploma.
Picha na FBM

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: Naibu Waziri wa Eilimu na Ufu...


Asalam alayqum, jamani poleni, inshalaah msichoke sana kwani muda si mrefu zoezi la kuwatunuku ndugu zetu vyeti litaanza, si mnaona jinsi Mc anavyopeleka shughuli harakaraka kwa kuzingatia muda uliosalia? inshalaah allah ataleta kheri katika siku hii ya leo, mwenye kufanya subira ametengewa haki yake na allah.
Picha na Ismail Mang'ola / FBM 


MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: Naibu Waziri wa Eilimu na Ufu...

Akina dada wa Kiislam wakisoma risala mbele ya Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi katika Mahafali ya kuwaaga wahitimu wa ualimu katika Chuo hicho.
Picha na Ismail mang'ola / FBM

MANG'OLA MEDIA .COM: Naibu Waziri wa Eilimu na Ufundi Mhe. Philiph Mulu...

Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhe. Philiph Mulugo wa pili kutoka kushoto akiwa pamoja na Viongozi wa Chuo cha Ununio chuo cha Kiislam wakisikiliza kwa makini risala iliyokuwa ikisomwa na mmoja wa wahitimu wakati wa Mahafali ya kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika May 20 mwaka huu Boko nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Picha na Ismail Mang'ola / FBM

MANG'OLA MEDIA .COM: Naibu Waziri wa Eilimu na Ufundi Mhe. Philiph Mulu...


Wahitimu wa Chuo cha Kiislam cha (Ununio Teachers College kiliuchopo Boko jijini Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini majibu ya risala iliyokuwa ikijibiwa na Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhe. Philiph Mulugo katika Mahafali yaliyofanyika Chuoni hapo May 20 mwaka huu. Picha na Ismail Mang'ola / FBM


Monday, May 21, 2012

Naibu Waziri wa Eilimu na Ufundi Mhe. Philiph Mulugo akisoma risala iliyoandaliwa na wahitimu wa chuo cha Kiislam cha Ununio wakati wa Mahafali ya kwanza chuoni hapo yaliyofanyika May 20 mwaka huu, chuo hicho kipo Boko nje kidogo ya jiji la Dar Es Salaam. Picha Na Ismail Mang'ola / FBM 

NAIBU WAZIRI WA ELIMU AHIMIZA NIDHAMU VYUONI

Na Ismail Mang'ola

 

Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhe. Philiph mulugo amehimiza nidhamu kuwepo vyuoni na kusema zaidi masomo ya maadili yawe nguzo ili kupunguza mmonyoko wa maadili ambao hivi sasa havishikiki.

Mhe. Mulugo amekipongeza chuo cha ualimu cha Ununio Teachers College kinachotoa mafunzo ya ualimu na kusema, wahitimu wa chuo hicho wananidhamu hajapata kuona.

Akitoa kauli hiyo kwenye Mahafali ya kwanza tangu kuanzishwa kwa chuo hicho mwaka 2010, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Chuoni hapo, Mulugo alisema amefarijika kuona wahitimu wakiwa na nidhamu pamoja na maadili mema aliyoyaona kwa wahitimu hao tofauti na alivyozoea kwa wahitimu wa vyuo vingine kwa kile alichodai kuwa kutokuwepo kwa zomeazomea katika chuo hicho.

Naibu huyo alisema walimu wanapaswa kusimama kidete kuhakikisha wanafundisha somo hilo ili kuinusuru familia zijazo ambazo hivi sasa baadhi ya jamii yetu imekuwa ikipotoka kwenye maadili huku wengine wakivaa milegezo hali ambayo inadhihirisha kuwa mtu huyo hakulelewa katika misingi yenye maadili.

Sambamba na hilo, mhe. Naibu Waziri pia amekitaka chuo hicho kuendeleza malezi mema kwa wanachuo wake na yenye kuzingatia mila na tamaduni ya kweli na kusisitiza walimu wa chuo hicho wasikome kufundisha suala zima la nidhamu kama walivyoanza hapo awali.

Naibu huyo alisema kwamba, kitendo cha wahitimu hao kupokea salamu za Takbir kama dini yao inavyowataka hakika kimemkuna kiasi cha nini afanye ili aweze kuwalipa fadhila za kujijenga kinidhamu kwa wahitimu hao, alibainisha Mhe. mulugo.

Aidha mhe. Mulugo amewataka wahitimu hao kuridhika na mazingira yoyote watakapopelekwa kufanya kazi bila kuangalia kuwa ni vijijini ama la, alisema hivi sasa walimu wengi wamekuwa wakikwepa kwenda kufundisha mikoani kwa kile alichidai kuwa ni mbali na familia zao zilipo.

Alisema endapo wahitimu hao kama watafuata mkumbo wa walimu wengine ambao wametokea katika vyuo ambavyo havifundishi masuala ya dini, hapo watakuwa wamepotea na watakuwa hawajaitendea haki taaluma yao kwani taaluma hiyo haichagui mahali pa kufanyia kazi wala eneo.

kutoka na nidhamu hiyo kwa wahitimu hao, mhe. mulugo alimtaka mwalimu anayefundisha somo la nidhamu aliyetambulika kwa jina la Ustadhi Juma nchia ambaye pia ni Makamu wa chuo, alimpongeza kwa jitihada zake hizo na kumpatia kiasi cha 30, 000 huku akimuahidi kitita kingine cha 470,000 kama motisha ya kutoa somo la maadili mema.

Hata hivyo Mhe. Mulugo ametoa onyo kali kwa wamiliki wa vyuo vyote ambavyo havina usajili na kutofuata taratibu, alisema endapo siku atakapobaini baina ya vyo hivyo, atavifungia na kuwanyang'anya leseni hali ambayo itawalazimu kutopata tena leseni ya kuanzisha vyuo.

 

Saturday, May 19, 2012

MANG'OLA MEDIA .COM: MANG'OLA MEDIA .COM: Hiki ni mojawapo ya chanzo ch...

Wanafunzi wa vyuo mbalimbali za Kiislam wakisikiliza kwa makini mada iliyokuwa ikizungumziwa juu ya Chaguzi zinavyotakiwa kufanyika na kuwachagua viongozi wao katika vyuo. mada hiyo ilitolewa na  
MANG'OLA MEDIA .

MANG'OLA MEDIA .COM: Hiki ni mojawapo ya chanzo cha maji kilichopo kati...

MANG'OLA MEDIA .COM: Hiki ni mojawapo ya chanzo cha maji kilichopo kati...: Hiki ni mojawapo ya chanzo cha maji kilichopo katika mlima KWARAA mradi uliokuwa  umeanzishwa na wananchi lakini baadaye kundi la watu ful...

Thursday, May 17, 2012

Hiki ni mojawapo ya chanzo cha maji kilichopo katika mlima KWARAA mradi uliokuwa  umeanzishwa na wananchi lakini baadaye kundi la watu fulani likajitokeza na kuwanyang'anya wananchi hao na kukiita GAWASA, kulia ni Bw. Dodoo aliyekuwa Mhasibu wa mradi wa maji kabla ya kunyang'anywa na Gawasa. Picha na Ismail Mang'ola / FBM.

Haya ni mandhari ya mikoa ya Kaskazini


Jamani sisi wa mjini achane tu tung'ang'anie huku mjini, hili ni bomba la maji safi linalogawa maji katika vijiji zaidi ya vinne, kibaya zaidi halina mfuniko pia liko porini kiasi ambapo ni hatari kwa wakazi wa vijiji vinavyotegemea maji hayo. Picha na Ismail mang'ola / FBM
 

Mkurugenzi wa Fullutamu.blogspot.com Bw. Ismail Mang'ola wa tatu kutoka kulia akiwa na washkaji zake katika picha ya pamoja kabla ya kifo cha aliyekuwa nguli wa filamu hapa bongo Steven Charles Kanumba walipokuwa katika ukumbi wa Diamond Jubilee wakati wa fainali ya Bongo Star Saech 2009. picha na Christopher Lisa/FBM


Licha ya kwamba banda hili ni kituo cha mbio za mwenge! lakini huwezi amini kwa nyakati zisokuwa rasmi hugeuzwa kama mahakama na baadhi ya wananchi wa mji wa Gallapo na vitongoji vyake wameshawahi kuhukumiwa katika banda hili na Mahakama ya Mwanzo Gallapo kwa madai ya kuharibu miundombinu ya maji. Picha na Ismail Mang'ola / FBM

Kutokana na uhaba wa maeneo ya malisho ya mifugo, Ng'ombe hawa hulazimika kufuata malisho juu ya mlima Kwaraa uliopo umbali mrefu kutoka kijiji cha ngaranaro Wilayani Babati Mkoa wa Manyara, hapa wapo juu ya mlima wakisaka majani. Picha na Ismail Mang'ola / FBM

Waskaji wakijiseveia kitoweo baada ya gari lililokuwa limebeba ng'ombe likitokea Mbagala kuwapeleka katika machinjio ya pugu kupata ajali katika makutano ya barabara ya Mandelea na Sokota. Picha na Ismail Mang'ola/FBM 

Msanii nguli wa maigizo Tuesday Kihangala 'Chuz akigombea ugali na msanii wake ofisini kwake mtaa wa Kambangwa Kinondoni jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Picha na Ismail Mang'ola/ FBM

Wakazi wa mji huu mdogo wa Kata ya Gallapo iliyopo katika Wilaya ya Babati Vijijini ukiwa katika muonekano wa picha, upo hatarini kupoteza maisha ya wakazi wake kutokana na Mamlaka ya maji safi na maji taka Gallapo Water Suplly GAWASA, kushindwa kuweka sawa miundombinu ya maji hayo kutokana na vyanzo vya maji hayo kutokuwa na mifuniko. Picha na Ismail Mang'ola/FBM.....Soma habari hiyo chini.

  • MAMLAKA YA MAJI GALLAPO YAHATARISHA MAISHA YA WAKAZI!
  • Wakazi waijia juu chombo hicho na kung’oa vyanzo vyao
  • Na Ismail Mang’ola – Babati
  • Mamlaka ya maji safi na maji taka ya mjini Gallapo inayodaiwa kuwa ni chombo cha kuungaunga kinachofanya kazi zake kimaslahi Gallapo Water Sapply GAWASA, imeelezwa kuwa chombo hicho kinahatarisha maisha ya wakazi wa mji huo pamoja na vijiji vingine vinaoutumia huduma ya maji kutoka chini ya usimamizi wa chombo hicho.
  • Wakizungumza na gazeti la KISIWA gazeti linalofanya utafiti wa kila aina, wakazi hao wa mjini Gallapo pamoja na baadhi ya vijiji wamesema kwamba, mamlaka hiyo imewaweka katika wakati mgumu baada ya kushindwa kuendesha huduma hiyo ambayo ilikuwa mali yao na kuwanyang’anya huku ananchi walioanzisha chombo hicho pamoja na vyanzo vya maji hayo.
  • Wakilizungumzia yukio hilo kwa masikitiko na mwandishi wa KISIWA, wananchi hao  walisema kuwa, mamlaka hiyo kabla ya kuwanyang’anya mradi wa  vyanzo hivyo maji hayakuwa ya shida kama ilivyo hivi sasa, kwani hapo awali maji yalikuwa yanatoka bila matatizo huku wananchi wakiwa wamejiwekwa malengo ambapo shilingi mia tano walipeleka kwenye mfuko wa maji na mia tano nyingine waliingiza kwenye mfuko wa kijiji, lakini hivi sasa hali ya upatikanaji wa maji hayo yamekuwa kama vile lulu.
  • waliendelea kulipasha Kisiwa na kusema kwamba, hivi sasa vyanzo vya maji hayo vilivyopo mlimani vipo wazi takribani miaka miwili sasa bila kufunikwa na mifuniko hali ambayo inawafanya baadhi ya vijana kuingia ndani ya chemba hizo na kuoga huku wakiwa na wasi wasi mkubwa kupoteza maisha endapo kama atatokea mtu na kuweka sumu.
  • Naye katibu kata wa CCM kata ya Gallapo alipotafutwa na mwandishi wa gazeti hili Bw. Hamisi Maneno alisema kuwa, kuachwa wazi kwa vyanzo hivyo ni hatari kubwa kwa maisha ya wakazi wa Gallapo na vijiji vingine ambavyo vinategemea maji hayo kutoka mlimani’ mlima wa KWARAA.
  • Alisema hatari iliyopo mbele yao ni kubwa na endapoa kama atatokea mtu mwenye sababu zake za kutaka kuondoka na wengi na akatumbukiza sumu, basi maafa yatakayotokea ni makubwa kutokana na vyanzo hivyo kuwa tegemezi kwa zaidi ya vijiji visivyopungua saba.
  • Alisema kuharibiwa kwa vyanzo hivyo na kupelekea kutoweka kwa amani baina ya Mamlaka hiyo na wanakijiji, ni njama za Diwani wa kata hiyo bw. Michael Naas Bim ambaye amekuwa kiranja wa mamlaka hiyo kutokana na maslahi ambayo wamejiwekea.
  • Alisema kabla ya kuingia kwa chombo hicho cha GAWASA, bei ya bili ya maji ilikuwa 1000, ambayo ililenga kwa mwananchi wa hali ya chini, lakini mara baada ya kuingia Gawasa, walipandisha kutoka 1000, 2000 hadi 3000 kitu ambacho kiliwafanya wananchi wengi washindwe kulipa bili kutoka na gharama hizo kupanda huku wakitambua kuwa upatikanaji wa maji hayo si ya shida kama ilivyo maeneo mengine ambapo hugharimu suala la umeme kuyavuta, alisema Maneno.
  • Bw. Maneno aliendelea kudai kwamba, kilichowauma zaidi wananchi hao kupandishiwa bili ya maji ni baada ya kutafakari namna walivyoyahangaikia kwa  kuuza mali zao Ng’ombe, Mbuzi, Mabati ya nyumba pamoja na mali zingine ambazo tayari vilikuwa vimeshanunuliwa kwa ajili ya matumizi yao binafsi huku watukufu waislam wakiwa katika mfungo wa mwezi mtukufu sambamba na akina mama ambao walikuwa wajawazito, wote kwa pamoja walijitolea kwa ajili ya kupata huduma hiyo iliyoitesa jamii ya kata hiyo pamoja na kata zingine kwa muda mrefu.
  • Katibu huyo aliendelea kulipasha Kisiwa na kusema kwamba, baada ya mamlaka hiyo kupandisha bei ya bili ya maji, wananchi waliijia juu na kuamua kuharibu vyanzo vyao vya maji hayo ambayo walianzisha wenyewe hali ambayo ilimpelekea Diwani wa kata hiyo ya Gallapo Bw. Michael Naas Bim kugeuka kiranja wa Gawasa na kuwakamata baadhi ya viongozi wa kata hiyo akiwamo katibu kata, mwenyekiti pamoja na wananchi wengine na kuwafungulia mashtaka.
  • Awali mwaka 2010 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Khalfani Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akiomba kura kuchaguliwa kwa mara nyingine alikitaka chombo hicho kianzishe vyanzo vyao badala ya kutumia vyanzo vya wananchi, lakini baada yam he. Kikwete kuwatupia kisogo hali iliendelea kubaki pale pale na mamlaka hiyo kuendeleza ubabe wao hali ambayo inawafanya wakazi hao kutokuwa na maelewano na mamlaka hiyo kwa kukataa kulipia bili ya maji na kusema hadi siku rais atakapofika kusuluhisha mgogoro huo.
  • Baada ya taarifa hiyo mwandishi wetu alimtafuta meneja wa mamlaka hiyo bw. Daniel Manimo ambaye alikiri kuwa kuwepo kwa mgogoro huo, Manimo alisema kwamba, baada ya chombo chao kuingia hapo walifanya mazungumzo na uongozi wa kata na walipokubaliwa walianza kazi kwa kushirikiana na wanakijiji hao lakini baada ya miaka miwili, wanakijiji hao walianza kukwepa kulipia bili ya maji hali ambayo ikawalazimu kuwakatia maji kwani, alisema kufanya hivyo ni kutokana na kukuza mradi huo ambao ulianzishwa chini ya kiwango.
  • Aliendelea kusema kwamba, baada ya wanakijiji hao kugoma kulipia maji na walipoanza zoezi la kuwakatia maji hayo, hivyo wanakijiji hao nao wakaanza kukata vyanzo hivyo hali ambayo iliwalazimu kuwakamata na kuwafungulia mashtaka.
  • Lakini cha kushangaza mnamo tarehe 12 April mwaka huu, mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. …. Aliwaita baadhi ya viongozi wa kata hiyo ambapo aliwaeleza kuwa chombo hicho hakikuwa rasmi na hivyo kuwataka viongozi wa mamlaka hiyo kufuta kesi iliyofunguliwa dhidi ya wananchi hao pamoja na viongozi wa kata ya CCM kata ya Gallapo na kuitaka mamlaka hiyo kuwalipa fidia ya uendeshaji kesi, kilisema chanzo hiki.  
  •  
Akina mama hawa wakazi wa kijiji cha Ngaranaro wilaya ya Babati, wakitoka kutafuta kuni kwa ajili ya matumizi ya kupikia kunihizo huzifuata umbali wa zaidi ya Km mbili katika mlima wa Haraa, huku wakizibeba kwa kutumia migongo yao. Picha na Ismail Mang'ola FBM.

MANG'OLA MEDIA .COM: KILA KUKICHA MOTO MOTO

 Wanafunzi wa Shule ya msingi Endanoga iliyopo katika kata ya Gallapo wilaya ya Babati vijijini mkoa wa manyara wakitoka shuleni wakielekea majumbani mwakwenda kula chakula cha mchana. Picha na Ismail mang'ola.