Thursday, May 17, 2012

Wakazi wa mji huu mdogo wa Kata ya Gallapo iliyopo katika Wilaya ya Babati Vijijini ukiwa katika muonekano wa picha, upo hatarini kupoteza maisha ya wakazi wake kutokana na Mamlaka ya maji safi na maji taka Gallapo Water Suplly GAWASA, kushindwa kuweka sawa miundombinu ya maji hayo kutokana na vyanzo vya maji hayo kutokuwa na mifuniko. Picha na Ismail Mang'ola/FBM.....Soma habari hiyo chini.

  • MAMLAKA YA MAJI GALLAPO YAHATARISHA MAISHA YA WAKAZI!
  • Wakazi waijia juu chombo hicho na kung’oa vyanzo vyao
  • Na Ismail Mang’ola – Babati
  • Mamlaka ya maji safi na maji taka ya mjini Gallapo inayodaiwa kuwa ni chombo cha kuungaunga kinachofanya kazi zake kimaslahi Gallapo Water Sapply GAWASA, imeelezwa kuwa chombo hicho kinahatarisha maisha ya wakazi wa mji huo pamoja na vijiji vingine vinaoutumia huduma ya maji kutoka chini ya usimamizi wa chombo hicho.
  • Wakizungumza na gazeti la KISIWA gazeti linalofanya utafiti wa kila aina, wakazi hao wa mjini Gallapo pamoja na baadhi ya vijiji wamesema kwamba, mamlaka hiyo imewaweka katika wakati mgumu baada ya kushindwa kuendesha huduma hiyo ambayo ilikuwa mali yao na kuwanyang’anya huku ananchi walioanzisha chombo hicho pamoja na vyanzo vya maji hayo.
  • Wakilizungumzia yukio hilo kwa masikitiko na mwandishi wa KISIWA, wananchi hao  walisema kuwa, mamlaka hiyo kabla ya kuwanyang’anya mradi wa  vyanzo hivyo maji hayakuwa ya shida kama ilivyo hivi sasa, kwani hapo awali maji yalikuwa yanatoka bila matatizo huku wananchi wakiwa wamejiwekwa malengo ambapo shilingi mia tano walipeleka kwenye mfuko wa maji na mia tano nyingine waliingiza kwenye mfuko wa kijiji, lakini hivi sasa hali ya upatikanaji wa maji hayo yamekuwa kama vile lulu.
  • waliendelea kulipasha Kisiwa na kusema kwamba, hivi sasa vyanzo vya maji hayo vilivyopo mlimani vipo wazi takribani miaka miwili sasa bila kufunikwa na mifuniko hali ambayo inawafanya baadhi ya vijana kuingia ndani ya chemba hizo na kuoga huku wakiwa na wasi wasi mkubwa kupoteza maisha endapo kama atatokea mtu na kuweka sumu.
  • Naye katibu kata wa CCM kata ya Gallapo alipotafutwa na mwandishi wa gazeti hili Bw. Hamisi Maneno alisema kuwa, kuachwa wazi kwa vyanzo hivyo ni hatari kubwa kwa maisha ya wakazi wa Gallapo na vijiji vingine ambavyo vinategemea maji hayo kutoka mlimani’ mlima wa KWARAA.
  • Alisema hatari iliyopo mbele yao ni kubwa na endapoa kama atatokea mtu mwenye sababu zake za kutaka kuondoka na wengi na akatumbukiza sumu, basi maafa yatakayotokea ni makubwa kutokana na vyanzo hivyo kuwa tegemezi kwa zaidi ya vijiji visivyopungua saba.
  • Alisema kuharibiwa kwa vyanzo hivyo na kupelekea kutoweka kwa amani baina ya Mamlaka hiyo na wanakijiji, ni njama za Diwani wa kata hiyo bw. Michael Naas Bim ambaye amekuwa kiranja wa mamlaka hiyo kutokana na maslahi ambayo wamejiwekea.
  • Alisema kabla ya kuingia kwa chombo hicho cha GAWASA, bei ya bili ya maji ilikuwa 1000, ambayo ililenga kwa mwananchi wa hali ya chini, lakini mara baada ya kuingia Gawasa, walipandisha kutoka 1000, 2000 hadi 3000 kitu ambacho kiliwafanya wananchi wengi washindwe kulipa bili kutoka na gharama hizo kupanda huku wakitambua kuwa upatikanaji wa maji hayo si ya shida kama ilivyo maeneo mengine ambapo hugharimu suala la umeme kuyavuta, alisema Maneno.
  • Bw. Maneno aliendelea kudai kwamba, kilichowauma zaidi wananchi hao kupandishiwa bili ya maji ni baada ya kutafakari namna walivyoyahangaikia kwa  kuuza mali zao Ng’ombe, Mbuzi, Mabati ya nyumba pamoja na mali zingine ambazo tayari vilikuwa vimeshanunuliwa kwa ajili ya matumizi yao binafsi huku watukufu waislam wakiwa katika mfungo wa mwezi mtukufu sambamba na akina mama ambao walikuwa wajawazito, wote kwa pamoja walijitolea kwa ajili ya kupata huduma hiyo iliyoitesa jamii ya kata hiyo pamoja na kata zingine kwa muda mrefu.
  • Katibu huyo aliendelea kulipasha Kisiwa na kusema kwamba, baada ya mamlaka hiyo kupandisha bei ya bili ya maji, wananchi waliijia juu na kuamua kuharibu vyanzo vyao vya maji hayo ambayo walianzisha wenyewe hali ambayo ilimpelekea Diwani wa kata hiyo ya Gallapo Bw. Michael Naas Bim kugeuka kiranja wa Gawasa na kuwakamata baadhi ya viongozi wa kata hiyo akiwamo katibu kata, mwenyekiti pamoja na wananchi wengine na kuwafungulia mashtaka.
  • Awali mwaka 2010 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Khalfani Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akiomba kura kuchaguliwa kwa mara nyingine alikitaka chombo hicho kianzishe vyanzo vyao badala ya kutumia vyanzo vya wananchi, lakini baada yam he. Kikwete kuwatupia kisogo hali iliendelea kubaki pale pale na mamlaka hiyo kuendeleza ubabe wao hali ambayo inawafanya wakazi hao kutokuwa na maelewano na mamlaka hiyo kwa kukataa kulipia bili ya maji na kusema hadi siku rais atakapofika kusuluhisha mgogoro huo.
  • Baada ya taarifa hiyo mwandishi wetu alimtafuta meneja wa mamlaka hiyo bw. Daniel Manimo ambaye alikiri kuwa kuwepo kwa mgogoro huo, Manimo alisema kwamba, baada ya chombo chao kuingia hapo walifanya mazungumzo na uongozi wa kata na walipokubaliwa walianza kazi kwa kushirikiana na wanakijiji hao lakini baada ya miaka miwili, wanakijiji hao walianza kukwepa kulipia bili ya maji hali ambayo ikawalazimu kuwakatia maji kwani, alisema kufanya hivyo ni kutokana na kukuza mradi huo ambao ulianzishwa chini ya kiwango.
  • Aliendelea kusema kwamba, baada ya wanakijiji hao kugoma kulipia maji na walipoanza zoezi la kuwakatia maji hayo, hivyo wanakijiji hao nao wakaanza kukata vyanzo hivyo hali ambayo iliwalazimu kuwakamata na kuwafungulia mashtaka.
  • Lakini cha kushangaza mnamo tarehe 12 April mwaka huu, mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. …. Aliwaita baadhi ya viongozi wa kata hiyo ambapo aliwaeleza kuwa chombo hicho hakikuwa rasmi na hivyo kuwataka viongozi wa mamlaka hiyo kufuta kesi iliyofunguliwa dhidi ya wananchi hao pamoja na viongozi wa kata ya CCM kata ya Gallapo na kuitaka mamlaka hiyo kuwalipa fidia ya uendeshaji kesi, kilisema chanzo hiki.  
  •  

No comments:

Post a Comment