Thursday, March 17, 2011

.Banza na Choki kunani?

  
Mafahari wawili ndani ya zizi moja, kulia ni Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki na kushoto ni Banza Stone mwanamuziki ghali hapa bongo.
Picha na Ismail Mang'ola.

Super Nyamwela akifanya vitu vyake kwa kushirikiana na madansa wenzake katika onyesho kali lililofanywa na kundi la Extra Bongo katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam.
RATIBA ya kundi zima la Extra Bongo wazee wa Vizigo kama vipi waite mabon town au ukuwapendelea zaidi unaweza ukawaita MJINI MIPANGO wanakushushia ratiba yao ya wiki watakapokuwa wanaporomosha burudani za kutosha ambazo kwa uhakika wengi wameweza kuzishuhudia.

Extra Bongo wiki hii wanatarajiwa kuimaliza hasa kwa kutumia zaidi Saikolojia. Ijumaa ya wiki hii wakali hao watashusha TSUNAMI ya kumalizia wiki katika ukumbi unaondana na wakati na uliotulia MEEDA uliopo Sinza jijini Dar es Salaam sambamba na nyimbo zao kali mpya ukiwemo MTENDA MTENDEWA.

RATIBA hiyo bado inasonga mbele ambapo siku ya Juma mosi kundi hilo litawasha moto mwingine katika ukumbi wa EQUATOR GRILL Mtoni kwa Azizi Ally.

KAMA KAWA ile siku ya Juma pili Kundi la EXTRA BONGO watafanya masababisho mengine katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni ambapo pia nyimbo kali zingine zitasikika siku hiyo, wakali wanaosababisha kunoga kwa muziki huo ni pamoja na nguli mwenyewe Ally Choki a.k.a Mzee wa Farasi ama Mzee Kijiko (GRADER), ama Mzee wa vibweka, usikubali kusimuliwa fika pale utakapowasikia wanatoa burudani.

No comments:

Post a Comment