Monday, March 28, 2011
Sunday, March 27, 2011
ZUNGU NDANI YA APRM
MHE. SHIBUDA NAYE AUKUBALI MPANGO HUO WA APRM.
WABUNGE SASA WAIKUBALI APRM.
HUU MKAKATI HUONDOA UMASIKINI JAMANIII!
HUU MPANGO MWENZIO NDIO KWANZA NAANZA KUUELEWA, KUMBE UNAMANUFAAE!
Mashirika, taasisi, Bunge waukubali mpango maridhawa wa APRM.
Thursday, March 17, 2011
UHAKIKA WA SIMBA KUNYAKUA UBINGWA HAUNA MAJADILIANO: RAGE
Kidoleni ana pete ya ndoa,Klabu yupo peke yake mbona mtihani kwa mama nanii. |
Wee Bi. Mkubwa! inamaana huna Hasband wako mahomu?.
Haya ni mambo ya wadau wa kumbi za burudani lakini mwenzangu na mie kama mambo haya huyahusudishi, hakiamungu huwezi kutoka hata kiduchu utaishia kuyasikia tu kwa wenzako lakini usipime. |
Aunt Ezekiel akiwa katika moja ya pozi. |
Msanii ghali wa muvi hapa tz Aunt Ezekiel akinena jambo na msanii mwenzake mishale ya saa tisa usiku katika ukumbi wa Mango jijini pale Twanga walipokuwa wakitoa burudani. Picha na Ismail Mang'ola. |
Mnenguaji wa Extra Bongo ambaye jina lake halikufahamika moja akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki katika moja ya onyesho la bendi hiyo hapa jijini. |
Kumbe Spaider nawe kwenye misafara ya Kenge umoooo! haya huku wapi tena, afu mbali kinoma na unakokaa duh.
Msanii wa muziki wa mduara Rashid Mustafa Msabaha (Spaider) kulia akiwa chobingo na mdu wake katika pande za Chang'ombe Unubini Temeke. |
Tuesday Kihangala akigombania ugali na Stella ambaye ni msanii wa muvi hapa bongo. |
.Banza na Choki kunani?
Mafahari wawili ndani ya zizi moja, kulia ni Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki na kushoto ni Banza Stone mwanamuziki ghali hapa bongo. Picha na Ismail Mang'ola. |
Super Nyamwela akifanya vitu vyake kwa kushirikiana na madansa wenzake katika onyesho kali lililofanywa na kundi la Extra Bongo katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam. |
Extra Bongo wiki hii wanatarajiwa kuimaliza hasa kwa kutumia zaidi Saikolojia. Ijumaa ya wiki hii wakali hao watashusha TSUNAMI ya kumalizia wiki katika ukumbi unaondana na wakati na uliotulia MEEDA uliopo Sinza jijini Dar es Salaam sambamba na nyimbo zao kali mpya ukiwemo MTENDA MTENDEWA.
RATIBA hiyo bado inasonga mbele ambapo siku ya Juma mosi kundi hilo litawasha moto mwingine katika ukumbi wa EQUATOR GRILL Mtoni kwa Azizi Ally.
KAMA KAWA ile siku ya Juma pili Kundi la EXTRA BONGO watafanya masababisho mengine katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni ambapo pia nyimbo kali zingine zitasikika siku hiyo, wakali wanaosababisha kunoga kwa muziki huo ni pamoja na nguli mwenyewe Ally Choki a.k.a Mzee wa Farasi ama Mzee Kijiko (GRADER), ama Mzee wa vibweka, usikubali kusimuliwa fika pale utakapowasikia wanatoa burudani.
Monday, March 14, 2011
HUWEZI AMINI!, HIVI ALIVYO ANATEGEMEWA NA MAMA YAKE MZAZI.
Mlemavu Balton Kiwelu ameelezea mstakabali wake juu ya hali aliyonayo na kusema licha ya ulemavu aliokuwa nao bado mama yake mzazi anamtegemea. Kiwelu amesema mama yake pia ni mlemavu ambaye alikatwa mguu wake mika mingi iliyopita na kumsababishia hali hiyo ya kutojishughulisha na badala yake akalitupia jicho lake kwa Balton. Watanzania, kutoa ni moyo, mwenye nacho asisite kumtafuta kwani anapatikana Liwiti / Msimbazi au barabara ya Bibi Titi Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Picha na Ismail Mang'ola.
SEMINA YA WABUNGE WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA UMEFUNGULIWA RASMI LEO.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe akizungumza na waandishi wa habari juu ya mustakabali wa kampuni tata ya kufua umeme DOWANS katika ukumbi wa Blue Peal Hotel ubungo Plaza jijini Dar es Salaam leo. Picha na Ismail Mang'ola.
Sunday, March 13, 2011
MTU MZIMA KAZINI
Huyu ni askari wa kikozi cha Zima moto. |
Picha na Ismail Mang'ola.
KILA KUKICHA MOTO MOTO
Gari lenye namba za usajili STK 2691 likiwa katika eneo la tukio mara baada ya kumaliza kuuzima moto huo. |
Baadhi ya wapangaji wakiwaomba maafisa wa jeshi la polisi hawapo pichani kuingi ndani kuangalia kama kuna baadhi ya vitu vyao vilivyosalimika. |
Abdkarim wa pili kutoka kushoto ambaye ni mfanyakazi wa Kampuni ya Bakharesa akihojiwa na maafisa wa jeshi la polisi, Tanesco na wengine kutoka kikosi cha Zima moto. Picha na Ismail Mang'ola |
Friday, March 11, 2011
EXTRA BONGO WAKALIA KITI CHA KIFALME
1.Kundi la muziki wa dansi hapa nchini Extra Bongo hivi sasa limekaa mahala pazuri baada ya kufanikiwa kukikalia kiti cha Kifalme kwa kuzikamata baadhi ya kanda zinazohusudu burudani hiyo hasa katika kanda za Tabata, Kawe na maeneo mengine.
2.Nguli wa miondoko ya dansi Ally Choki akiwaburudisha mashabiki wa muziki huo katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam. Picha na Ismail Mang'ola.
2.Nguli wa miondoko ya dansi Ally Choki akiwaburudisha mashabiki wa muziki huo katika ukumbi wa Mango Garden Kinondoni jijini Dar es Salaam. Picha na Ismail Mang'ola.
Thursday, March 10, 2011
Subscribe to:
Posts (Atom)