Tuesday, March 15, 2016

True value Media: True value Media: True value Media: MSIMAMO MEDIA ...


















































Tuesday, March 15, 2016






Maboresho ya Uwanja wa Uhuru yanaendelea vizuri na kuridhisha


Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Makoye Alex Nkenyenge akielekeza

jambo kuhusu wavu uliowekwa kwa ajili ya kuzuia mashabiki wasirukie na kuharibu

miundombinu katika maeneo ya vyoo vya uwanja wa Uhuru jana wakati wa kikao cha

ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo.
 
Msanifu wa Majengo na mbunifu wa Mchoro wa Uwanja wa Taifa Aloyce Peter Mushi

akifafanua jambo wakati wa kikao cha ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo jana

jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Bibi.

Cecilia Kasongo, Mhandisi wa Uwanja wa Taifa Yusuf, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya

Michezo Makoye Alex Nkenyenge, Muhandisi wa mradi wa ujenzi wa uwanja wa Uhuru E.

Mwamakunga na Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio.

Meneja wa Ujenzi wa Kampuni ya BCEG inayojenga uwanja wa Uhuru Zhang Jiawei

akifafanua jambo wakati wa kikao cha ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo jana

jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo

Makoye Alex Nkenyenge, Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio, Msanifu wa Majengo na

mbunifu wa Mchoro wa Uwanja wa Taifa Aloyce Peter Mushi Muhandisi wa mradi wa ujenzi

wa uwanja wa Uhuru E. Mwamakunga.
Wajumbe wa kikao cha kukagua na kutathmini maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa

Uhuru wakikagua miunndombinu ya majitaka inayoendelea kujengwa katika uwanja wa

Uhuru jana jijini Dar es Salaam. 
 
Meneja wa Uwanja wa Taifa Rish Urio(mwenye suti nyeusi) akielezea jambo wakati wa

kikao cha ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja wa Uhuru jana jijini Dar es Salaam. 
 
Muonekano wa nje wa Uwanja wa Uhuru.

Picha na Frank Shija.




Serikali yawapongeza wadau wa afya katika mapambano ya Ugonjwa wa Kisukari nchini

Na Ismail Mang'ola 


Serikali
imewapongeza wadau kwa kutoa huduma za chanjo ya ugonjwa wa Kisukari
ikiwemo kusaidia vijana wadogo wanaosomea masomo mbalimbali ya kisayansi
hapa nchini.




Akizungumza
wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la tatu la ugonjwa wa Kisukari
kwa nchi za Afrika Mashariki,Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya na
Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi
Kigwangalla, amebainisha kuwa Serikali kupitia wizara hiyo ina mpango
kabambe wa kuhakikisha inapambana na tatizo la ugonjwa wa Kisukari hapa
nchini ambapo pia amewataka wadau wasichoke kushirikiana katika
mapambano hayo.
Aidha,
amewapongeza vijana walio katika vyuo vikuu hapa nchini licha ya kupata
tiba ya ugonjwa wa Kisukari, lakini kwa hali yao hiyo bado wana moyo wa
kusoma kuhakikisha wanafika mbali hivyo Serikali inajisikia faraja na
kuwataka wadau kuwa na moyo huo huo wa kusaidiana na Serikali.
 
Mgeni
rasmi, Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na
Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa hotuba maalum ya uzinduzi wa
kongamano hilo.



Kwa
upande wao baadhi ya washiriki wakiwemo vijana wanafunzi na wengine
wakiwemo waliotoa igizo namna ya ugonjwa Kisukari jamii unavyouweka
kando, wameeleza kuwa kitendo cha dozi ya Kisukari kuuzwa kinawapa shida
watu wengi kwani wapo wanaopoteza maisha kwa kukosa pesa za kutumikia
dozi hiyo.



Hata
hivyo, walimuomba Naibu Waziri Dk. Kigwangalla kuhakikisha Serikali
wanaliangalia hilo ili dozi ya Kisukari yaani Insulini, ipatikane bure
kwa watumiaji wake.
Kongamano
hilo lililozinduliwa jana Machi 14.2016, ni la siku tatu na
linatarajiwa kufikia tamati, kesho Machi 16.2016. Ambapo linajumlisha
wataalaam wa utafiti wanasayansi katika ugonjwa wa Kisukari ( pre –
congress training – applied research in diebetes) na kuandaliwa na asasi
inayojulikana kama (EADSG) The Eafrica diabetes study group. 
 
Baadhi
ya wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu ambao ni wadau wakubwa katika
mapambano dhidi ya Kisukari wakiwa tayari kutoa ujumbe kwa Serikali
kuona namna ya kusaidia jamiii katika mapambano ya ugonjwa wa kisukari.
Asas hii ilianzishwa mwaka 2011 ili kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa huo na kuutafiti pamoja na kutafuta tiba.


Awali
akiongea na waandishi wa Habari, Mratibu wa Kongamano hilo Doctor
Kaushik Ramalya, amesema wageni mbalimbali wapo katika majadiliano na
uchunguzi huo wa Kisayansi, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu wa
namana ya kutua matatizo yatokanayo na ugonjwa huo.
 
Mtaalam
na Mwanasayansi wa magonjwa ya Kisukari kutoka nchini India,Bw.Anil
Kapur (MDI) akiwasilisha mada na utafiti juu ya magonjwa hayo ya
Kisukari



UTAFITI:


Aidha
utafiti uliotolewa hivi karibuni umeonyesha kuwa katika kila sekunde
sita mtu mmoja hufa kutokana na ugonjwa wa kisukari ( vifo zaidi ya
milioni 5.0 hutokea duniani). Mmoja katika watu wazima 11 ana ugonjwa wa
kisukari ( watu milioni 415 duniani kote wanaishi na Kisukari). 
Moja
katika vizazi saba, huadhirika na ugonjwa wa kisukari katika kipindi
cha ujauzito na kujifungua.Robo tatu (75%) ya watu wenye ugonjwa wa
kisukari wanaishi katika nchi chini na kipato cha kati. 
Zaidi
ya watu wazima wengi wanakufa kutokana na ugonjwa wa kisukari kuliko
kutokana na VVU / UKIMWI, kifua kikuu na hata malaria.wastani wa milioni
14.2 watu wazima wenye umri kati ya 20-79 wana ugonjwa wa kisukari
katika Kanda ya Afrika. 
Afrika
inaongoza kwa wagonjwa wa kisukari ambao haujatambuliwa, kutokana na
kutocheki afya zao; zaidi ya 66.7 % ya watu wenye ugonjwa wa kisukari
hawajui kuwa wana ugonjwa wa kisukari. 
Mtu
ana kisukari aina ya 2 (Type 2 Diabetes) anaweza kuishi kwa miaka
kadhaa bila kuonyesha dalili yoyote, madhara yanayoweza kujitokeza ni
pamoja na ugonjwa wa figo , moyo kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa
jicho na kusababisha upofu na matatizo ya mguu na kusababisha ulema.
Mataifa
ya Afrika kwa idadi kubwa ya watu wenye ugonjwa wa kisukari ni pamoja
na Afrika Kusini (2.3 milioni ), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (1.8
milioni ) , Nigeria ( milioni 1.6 ) na Ethiopia (1.3 milioni).
Mkurugenzi
msaidizi wa magonjwa yasiyoambukizwa katika Wizara ya Afya,Prof. Ayoub
Magimba akimkaribisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla
(Hayupo pichani).
Baadhi
ya wanafunzi na vijana ambao wapo katika mpango wa Kisukari wakiwa
tayari kutoa ujumbe kwa Serikali kuona namna ya kusaidia jamiii katika
mapambano ya ugonjwa wa kisukari.
Vijana wanaosoma masomo ya sayansi na pambano ya ugonjwa huo wa Kisukari
Dk.Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo..
Dk.Kigwangalla akiwa na vijana hao
Dk.
Kigwangalla akiwa na vijana wakati wa tukio hilo la ufunguzi rasmi wa
kongamano la kisayansi kwa nchi za Afrika Mashariki dhidi ya magonjwa ya
Kisukari
Vijana wakiwasilisha mada.
Dk. Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washirikiDk. Kigwangalla akiwa na baadhi ya washiriki hao kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki 
Vijana
washiriki wakionesha igizo la namna ya Jamii wanavyochukulia ugonjwa
huo ikiwemo suala la kuamini nguvu za giza. Hata hivyo jamii imetakiwa
kuchukua hatua ikiwemo kutembelea Hospitali ilikupata tiba sahihi ya
wataalam wa Hospitali.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mkutano huo
Baadhi
ya washiriki ikiwemo viongozi na wadau wakubwa wa magonjwa ya Kisukari
wakiwa katika meza kuu wakifuatolia hotuba ya mgeni rasmi (Hayupo
pichani).
Mgeni rasmi, Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla akisalimiana na wageni wengine waalikwa katika mkutano huo
Mgeni rasmi, Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla akisalimiana na wageni wengine waalikwa katika mkutano huo
Mgeni rasmi, Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla akisalimiana na wageni wengine waalikwa katika mkutano huo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri, Dk. Kigwangalla akiwasilia kufungua rasmi kongamano hilo
Dk.
Kigwangalla akipata picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wanaosomea
masomo ya Sayansi na udaktari ambao wanapambana na magonjwa ya Kisukari.
Dk. Kigwangalla aliwapongeza wanafunzi hao kwa juhudi zao hizo ambapo
amewahakikishia juu ya Serikali kuwa na mipango endelevu ikiwemo
kuwaendeleza zaidi kwa kushirikiana na wadau na wafadhiri mbalimbali.
Dk.
Kigwangalla akipata picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wanaosomea
masomo ya Sayansi na udaktari ambao wanapambana na magonjwa ya Kisukari.
Dk. Kigwangalla aliwapongeza wanafunzi hao kwa juhudi zao hizo ambapo
amewahakikishia juu ya Serikali kuwa na mipango endelevu ikiwemo
kuwaendeleza zaidi kwa kushirikiana na wadau na wafadhiri mbalimbali.
Dk.
Kigwangalla akiagana na viongozi mara baada ya kumaliza kwa ufunguzi wa
kongamano hilo linaloendelea leo na kufikia tamati hiyo kesho Machi
16.2016. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).




MWANAMKE WA AFRIKA BADO ANAKABILIWA NA CHANGAMOTO - WAZIRI UMMY MWALIMU


Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Ally
Mwalimu ( Mb) akitoa hutuba kwa niaba ya Kundi la Nchi za Afrika wakati
wa ufunguzi wa Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu
Hali ya Wanawake ( CSW).Mkutano huu wa wiki mbili unawakusanya
wawakilishi kutoka serikali mbalimbali duniani na Asasi za Kiraia ambapo
hujadiliana na kubalishana uzoefu na kuelimishana kuhusu hatua
mbalimbali ambazo serikali zao zinachukua katika kuboresha maisha ya
mwanamke na mtoto wa kike.
Waziri wa Malawi akimpongeza Waziri Ummy Mwalimu mara baada ya hotuba yake aliyoitoa kwa niaba ya Kundi la Nchi za Afrika.
Mhe.
Waziri Mwalimu akichangia majadiliano ya Mawaziri yaliyofanyika mara
baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 60 wa Kamisheni kuhusu hali ya Wanawake.
Majadiliano hayo ya Mawaziri yalihusu uimarishaji wa mfumo ya
kisheria na kisera kwaajili na utekelezaji wa usawa wa jinsia na
uwezeshaji wa wanawake.


Sehemu ya Washiriki wa Mkutano huo.

New York, Marekani
  Ismail Mang'ola na mashirika ya Kimataifa
 

Wakati
mamia ya wanawake   kutoka serikalini na  Asasi za Kiraia  wakiwa
wanakutana hapa Umoja wa Mataifa kwa mkutano wao  unaojadili hali yao
katika  maeneo mbalimbali. Mamia mengine ya wanawake  hususani  wale  wa
Afrika  wanaendelea kukumbana na changamoto lukuki zinazowarudisha
nyuma kimaendeleo.




Ni
wanawake hao wanaoishi katika  nchi zenye migogoro, vita visivyokwisha,
wenye kukabiliwa  na uhaba na ukosefu  mkubwa wa chakula, maji safi na
salama,  matatizo yatokanayo na  mabadiliko ya tabia nchi,  ndio ambao
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto,Mhe.  Ummy
Ally Mwalimu(Mb) ameitaka jumuiya ya kimataifa kuongeza kasi ya
 ushirikiano ili   malengo mapya ya maendeleo endelevu (Agenda 2030)
 yaweze kuwafikia.




Waziri
 Mwalimu ametoa wito huo jana jumatatu,  wakati alipotoa hutuba kwa
niaba ya nchi Afrika   katika  siku ya  kwanza ya Mkutano wa  60 wa
Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya wanawake (CSW) ambao
umeanza  hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.




Changamoto
hizo pamoja na nyinginezo nyingi zikiwamo  kutopata fursa ya  huduma za
afya ya uzazi  salama, elimu na usawa wa kijinsia  zinamfanya mwanamke
wa Afrika ashindwe kushindana na  wanawake wenzie hususani  wale walioko
katika  mataifa yaliyoendelea.  




Waziri
Mwalimu ambaye anaongoa ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu wa wiki
mbili,  alitoa hotuba hiyo kwa  niaba ya nchi za Afrika  kutokana na
kwamba Tanzania kupitia  Uwakilishi wake wa Kudumu wa Tanzania katika
Umoja wa Mataifa ni  Mwenyekiti wa Kundi  la Nchi za Afrika kwa mwezi
huu wa March.




Amewaeleza
washiriki wa mkutano huo waliofurika katika Ukumbi  Mkuu wa Mikutano wa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kwamba.  Ingawa pamekuwamo na
 makubaliano  na  mapendekezo mengi kuanzia yale yaliyofikiwa huko
Beijing, bado mwanamke anayeishi katika nchi zenye migogoro na vita
barani Afrika  ataendelea kuachwa nyuma na hivyo kukosa fursa ya
kushinda na wenzie.





Ingawa  vita,   ukame wa kutisha,  ukosefu  wa chakula, ukosefu wa maji
safi, ukichanganya na ukosefu wa  fursa za kiuchumi,  kijamii  na
kisiasa ni matatizo yanayowakabili watu maskini lakini mwanamke ndiye
anayeathirika zaidi” akaeleza Waziri Mwalimiu.




Na
kuongeza kwamba Afrika inaendelea kutilia mkazo hoja   ya
kuwashirikisha wanawake katika   majadiliano na utoaji wa maamuzi katika
masuala yanayowagusa yakiwamo masuala yanayohusu mabadiliano ya tabia
nchi na usuluhishi wa migogoro. 




Akaeleza
kwamba,  nchi zinazoendelea na zilizoendelea   zinapashwa  kuongeza
kasi ya ushirikiano  na ubia  baina yao ili kufanikisha utekelezaji
 Agenda 2030), Makubaliano  juu  Mabadiliko ya  Tabia nchi yaliyofikiwa
 huko Paris Ufaransa mwaka jana   na  makubaliano  yaliyofikiwa na
waafrika wenye kupitia Ajenda 2063 , ili  katika umoja wake dunia basi
iweze kumwondoa mwanamke na jamii nzima kutoka hapa ilipo na kufikia
hali bora  zaidi ya maisha.




Kama
 hiyo  haitoshi Waziri  amesema, Afrika inaamini pia katika uwezeshwaji
wa Sekta binafsi,  kupanua wigo wa  ujasiliamali kama njia moja wapo ya
kukuza uchumi endelevu , usawa wa kijamii,  usawa wa jinsia, ulinzi wa
mazingira na uwezeshaji wa mwanamke. 




Mada
kuu ya Mkutano wa 60 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya
Wanawake, ni “Uwezeshaji wa Wanawake na uhusiano wake na Ajenda 2030.




Awali
akizungumza mwanzoni mwa mkutano huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,
 Ban Ki   Moon amasema  tangu alipoingia madarakani mwaka 2006
amejjitadi kuongeza nafasi za viongozi wanawake katika Idara za
Sekreatarieti ya Umoja wa Mataifa.




Akitilia
msisitizo  hoja na haja ya kupanua wigo  wa wanawake kushika nafasi
katika ngazi za juu za maamumizi, Ban Ki Moon amesema, ingawa  nchi
nyingi  zimejitahidi sana kuongeza ushiriki wa wanawake katika nafasi za
juu za uongozi bado kuna  Nchi Tano ambazo hazina wanawake katika
 Mabunge  yao    ili hali Nchi nyingine 7 hazina mawaziri wanawake
katika serikali zao.




Naye
 Rais wa Baraza Kuu la 70 la  Umoja wa Mataifa  Bw Monges Lykketoft,
akizungumza wakati wa mkutano huo,  pamoja na kusisitiza umuhimu wa
utekelezaji wa Agenda 2030 ambayo ameitaja  kuwa ni jumuishi ameendelea
kupigia  chapuo la kutaka   Katibu Mkuu  ajaye wa Umoja wa Mataifa awe
 Mwanamke.




ZIARA YA WAZIRI MKUU, MAJALIWA WILAYA YA MISSENYI MKOANI KAGERA


Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shehena ya sukari wakati alipotembelea
ghala la kiwanda cha Sukari cha Kagera akiwa katika ziara ya mkoa wa
Kagera Machi 14, 2016.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua eneo la mpaka kati ya Tanzania na Uganda
kwenye Ranchi ya Missenyi mkoani Kagera Machi 14, 2016. Kushoto ni Mkuu
wa Wilaya ya Missenyi,Festo Kiswaga.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Uganda waishio kwenye
mpakani waliovuka mpaka ili kumuona wakati alipotembelea kijiji cha
Benkoma wialyani Missenyi akiwa katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14,
2016.
Baadhi
ya wananchi wa Uganda waishio mpakani wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa wakati alipotembelea kijiji cha Benkoma wilayani Missenyi akiwa
katika ziara ya mkoa wa Kagera Machi 14, 2016. Wananchi hao wa Uganda
walivuka mpaka ili kumuona Waziri Mkuu.


Waziri
Mkuu, Kassim Majajaliwa akifurahia zawadi ya picha aliyozawadiwa na
wananchi wa Kata ya Kakunyu wilayani Missenyi akiwa katika ziara ya mkoa
wa Kagera Machi 14, 2016.


Afisa
Mifugo wa Kata ya Kakunyu wilayani Missenyi, Eric Kagoro akitoa
maelezo mbele ya Waziri Mkuu na wananchi kuhusu tuhuma kuwa analinda
wafugaji toka nchi jirani wanaolisha mifugo yao kwenye ardhi ya Tanzania
kinyemela. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Monday, March 14, 2016






NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT KIGWANGALLA AZINDUA KONGAMANO LA TATU LA WANASAYANSI WA UGONJWA WA KISUKARI LEO JIJINI DAR




Naibu

Waziri wa Afya, Dkt Hamisi Kigwangalla katika ufunguzi wa Kongamano la
tatu la Kisanyansi na Utafiti wa ugonjwa wa kisukari Africa,
lililozinduliwa leo katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere
(JNICC),Kongamano hilo ambalo litamalizika tarehe 16 March 2016,
linaendeshwa na Asasi inayojihusisha na Masuala ya Ugonjwa wa kisukari
Afika Mashariki na Kusini,asasi inayojulikana kama (EADSG) The Eafrica
diabetes study group.Asas hii ilianzishwa mwaka 2011 ili kuhamasisha
jamii kuhusu ugonjwa huo na kuutafiti pamoja na kutafuta tiba.Kushoto
kwake ni Mratibu wa Kongamano hilo Doctor Kaushik Ramaiya,na baadhi ya
wageni kutoka Mfuko wa kusaidia Kisukari Duniani (NCD Symposium),kutoka
Denmark.
 

Kongamano la tatu la Wanasanyansi wa ugonjwa wa kisukari limezinduliwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Dkt Hamisi Kigwangalla katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere (JNICC)

Kongamano hilo ambalo litamalizika tarehe 16 March 2016, linaendeshwa na Asasi inayojihusisha na Masuala ya Ugonjwa wa kisukari Afika Mashariki,asasi inayojulikana kama (EADSG) The Eafrica diabetes study group.Asas hii ilianzishwa mwaka 2011 ili kuhamasisha jamii kuhusu ugonjwa huo na kuutafiti pamoja na kutafuta tiba.

Akiongea na waandishi wa Habari, Mratibu wa Kongamano hilo Doctor Kaushik Ramalya, Kongamano hilo limekaribisha wageni kutoka nchi nyingine za Afrika ya Mashariki na kusini kushiriki katika majadiliano na uchunguzi huo wa Kisayansi, ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu wa namana ya kutua matatizo yatokanayo na ugonjwa huo.

Alisema kongamano hilo ambalo linahusisha East African Diabetes study Group (EADSG) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, litafuatiwa na mkutano Maalum wa wadau wa kisukari duniani utakaofanyika, Machi 17 hadi 18 2016 katika ukumbi huo huo wa Kimataifa wa Julius Nyerere Convention Centre jijini Dar Es Salaam, Tanzania.

Mkutano huo ulioandaliwa na Mfuko wa kusaidia Kisukari Duniani (NCD Symposium),kutoka Denmark kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto nchini Tanzania, pamoja na Shirika la Afya Duniani Ofisi za Mikoa kwa Afrika pamoja na Shirikisho la Kisukari duniani utajadili mambo mbali kuhusu namna ya kusaidia wagonjwa wa ishio na Kisukari kwa kuwa gharama zake ni kubwa mno.

Mikutano hiyo miwili inalenga kutatua tatizo kubwa la Kisukari linalooendela kukua barani Afrika kwa sasa ambalo limeonekana kukua mara tatu zaidi ndani ya miaka mitano iliyopita.
Dk. Kaushik alisema kuwa, mbali na mjadala wa uchunguzi wa kisayansi, Mambo mengine yatakayo jadiliwa ni pamoja na

• Kuongezeka kwa ugonjwa wa kisukari katika nchi zinazoendelea, na lengo hasa juu Africa na namna ya kutatua matatizo yatokanayo.
• Kujadili kuhusu mzigo wa kijamii na kiuchumi unaotokana na watu wenye ugonjwa wa kisukari , familia zao na jamii kwa ujumla.
• Umuhimu wa kutafuta ufumbuzi wa Ugonjwa huu.
• Taarifa za uchunguzi za wataalam ngazi za mkoa.

Aidha utafiti uliotolewa hivi karibuni umeonyesha kuwa katika kila sekunde sita mtu mmoja hufa kutokana na ugonjwa wa kisukari ( vifo zaidi ya milioni 5.0 hutokea duniani)
- Mmoja katika watu wazima 11 ana ugonjwa wa kisukari ( watu milioni 415 duniani kote wanaishina Kisukari)
- Moja katika vizazi saba, huadhirika na ugonjwa wa kisukari katika kipindi cha ujauzito na kujifungua.
- Robo tatu (75%) ya watu wenye ugonjwa wa kisukari wanaishi katika nchi chini na kipato cha kati.
- Zaidi ya watu wazima wengi wanakufa kutokana na ugonjwa wa kisukari kuliko kutokana na VVU / UKIMWI, kifua kikuu na hata malaria.

- wastani wa milioni 14.2 watu wazima wenye umri kati ya 20-79 wana ugonjwa wa kisukari katika Kanda ya Afrika.
- Afrika inaongoza kwa wagonjwa wa kisukari ambao haujatambuliwa, kutokana na kutocheki afya zao; zaidi ya 66.7 % ya watu wenye ugonjwa wa kisukari hawajui kuwa wana ugonjwa wa kisukari.

- Mtu na kisukari aina ya 2 (Type 2 Diabetes) anaweza kuishi kwa miaka kadhaa bila kuonyesha dalili yoyote, madhara yanayoweza kujitokeza ni pamoja na ugonjwa wa figo , moyo kushindwa kufanya kazi, ugonjwa wa jicho na kusababisha upofu na matatizo ya mguu na kusababisha ulema.

- Mataifa ya Afrika kwa idadi kubwa ya watu wenye ugonjwa wa kisukari ni pamoja na Afrika Kusini (2.3 milioni ), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (1.8 milioni ) , Nigeria ( milioni 1.6 ) na Ethiopia (1.3 milioni).





SHULE YA MSINGI MBAGALA MAJIMATITU YACHIMBIWA VISIMA VYA MAJI.


Msimamizi wa
mradi wa uchimbaji wa visima vya maji katika Shule ya Msingi Mbagala majimatitu
kutoka DAWASA Muhandisi Abel Chibelela akiangalia maendeleo ya kisima kimoja
kati ya viwili vinavyochimbwa na Wakala wa Uchimbaji wa Visima na Mabwawa
(DDCA) katika shule hiyo kwa gharama ya shilingi milioni 24.5.


Wataalam
kutoka Wakala wa Uchimbaji wa Visima na Mabwawa (DDCA) wakiendelea kuchimba
kisima chenye urefu wa mita 130 katika shule ya Msingi Mbagala majimatitu,
Temeke jijini Dar es salaam.
Msimamizi
wa mradi wa uchimbaji wa visima vya maji katika Shule ya Msingi Mbagala
majimatitu kutoka DAWASA Muhandisi Abel Chibelela na Mhandisi Elizabeth Kingu, Katibu
Tawala Msaidizi Huduma za Maji (kushoto) wakiangalia maendeleo ya moja ya
kisima kinavyochimbwa na Wakala wa Uchimbaji wa Visima na Mabwawa (DDCA) katika
shule hiyo kwa gharama ya shilingi milioni 24.5.



Na. Aron Msigwa –Dar es salaam.


Walimu na
wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbagala Majimatitu iliyoko Temeke jijini Dar es
salaam watanufaika na huduma ya maji safi kufuatia Serikali kutoa kiasi cha
shilingi milioni 24.5 kwa lengo la kufanikisha mradi wa uchimbaji wa visima
viwili kwa lengo la kuboresha taaluma na mazingira ya shule hiyo.
Akizungumzia
uchimbaji wa visima hivyo leo jijini Dar es salaam msimamizi wa mradi huo kutoka Mamlaka ya Maji Safi
na Maji Taka (DAWASA) Muhandisi Abel Chibelela amesema kuwa kuchimbwa kwa
visima hivyo ni utekelezaji wa agizo la Serikali kuitaka DAWASA kutafuta vyanzo
vya maji katika shule hiyo ili kuwaondolea adha ya uhaba wa Maji.

Amesema shule
hiyo imekuwa na tatizo hilo kufuatia kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wapatao 6000
inayozidi uwezo wa miundombinu iliyopo sasa ikiwemo kisima kinachotumiwa na
wanafunzi hao kinachozalisha lita 8000 kwa siku wakati mahitaji halisi ya maji ni
Lita 40,000 kwa siku.

Amesema
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) kupitia Wakala wa Uchimbaji wa Visima
na Mabwawa ( DDCA) ilipewa jukumu la kuchimba visima viwili  vya shule hiyo kwa thamani ya shilingi
milioni 24.5 zikiwa ni gharama za uchimbaji, usafishaji wa visima hivyo na
gharama za vipimo vya maabara ili kuangalia ubora wa maji hayo.

" Kazi ya
uchimbaji wa visima hivi vyenye urefu wa mita 130 na 140 imeanza rasmi na
itachukua siku 14, tunafanya haraka ili tuweze kujua wingi wa maji yaliyopo na
ubora wake kama inafaa kwa matumizi ya binadamu"

Pia amesema
DAWASA itasimamia ujenzi wa minara mirefu ya matenki na kuongeza matenki
makubwa yatakayokidhi mahitaji ya shule hiyo yenye uwezo wa kuhifadhi maji lita
20 kwa kila shule.

Kwa upande
wake Mtaalamu kutoka Wakala wa Uchimbaji wa Visima na Mabwawa (DDCA) ambayo
ndiyo iliyopewa jukumu la kuchimba visima hivyo na DAWASA Bw. Nungwe Gwaga
akizungumzia uchimbaji wa visima hivyo amesema kuwa wao kama wataalam wa
kuchimba visima walifanya utafiti katika eneo hilo na kujiridhisha kuwa eneo la
shule ya Msingi Mbagala Maji Matitu lina Maji ya kutosha.

" Sisi
kama wataalam tulifanya utafiti (Physical Survey) katika eneo hili ili kujua
kama kuna maji na miamba inayopita pale pamoja na umbali wake, sisi
tumejiridhisha tutachimba mita 130 ambazo tayari zimetupa majibu ya kuwepo kwa
Maji "

Mwalimu Mkuu wa
Shule hiyo Bw. Abdul Mgomi akifafanua kuhusu visima hivyo amesema vitawezesha shule
yake kuondokana na adha ya uhaba wa huduma ya maji inayowakabili wanafunzi
shuleni hapo kufuatia mwitikio wa wazazi kuwaandikisha watoto wao shuleni hapo
kwa mwaka 2016.

Amesema kwa
sasa shule hiyo inatumia kisima kidogo chenye uwezo wa kuzalisha lita 8000 kwa
siku ikilinganishwa na mahitaji halisi ya lita 32000 kwa wanafunzi 6000
wanaosoma shuleni hapo.

Mwalimu Mgomi
ameshukuru jitihada zilizofanywa na viongozi wa mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa
na aliyekuwa Mkuu wa mkoa huo Mhe. Said Mecki Sadiki kwa kuwezesha upatikanaji
wa fedha za kuchimbia visima hivyo.

Ameeleza kuwa
mara baada ya visima hivyo kukamilika 
uongozi wa shule utaweka utaratibu wa matumizi ya maji hayo kwa shule na
ziada itakayopatikana na maji itauzwa kwa majirani wanaoishi kuzunguka shule
hiyo ili mradi uweze kujiendesha wenyewe.

Aidha, amesema
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea kuifanyia kazi
changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa shuleni hapo kwa kujenga mapya 10 ili
kukidhi mahitaji ya wanafunzi 6000 waliopo shuleni hapo pamoja na ujenzi wa shule
nyingine 2 zitakazoondoa kabisa tatizo la mrundikano wa wanafunzi.

Naye mmoja wa
Wazazi na Mjumbe wa Kamati ya Miradi ya shule hiyo Bi.Happiness Mgulambwa
akizungumza katika eneo vinapochimbwa visima hivyo ameishukuru Serikali kwa
kusikia kilio cha wazazi na wanafunzi hao kwa kuamua kuwachimbia visima hivyo
huku akiongeza  kuwa upatikanaji wa
huduma ya maji shuleni hapo utaongeza ufanisi kwa walimu na wanafunzi.

Amesema wao
kama Wazazi kupitia kamati ya miradi ya shule hiyo waliiomba Serikali kuwasaidia
kupata maji kwa wanafunzi shule hiyo  ili
kuondoa kero ya maji jambo ambalo lilikubaliwa.

" Kweli
wanafunzi wa shule hii walikua wanapata shida,uhaba wa maji hapa shuleni
uliwalazimu kuja na maji kwenye madumu jambo liliowafanya wakati mwingine
kufika wamechoka na hata kuchafuka, tunaishukuru sana Serikali yetu ya awamu ya
tano kwa kutusaidia" Amesema Bi.Mgulambwa. 

MIWISHO.





No comments:

Post a Comment